WAKATI
Haruna Niyonziam akiwa amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea
Yanga, habari zilizotufikia hivi punde zinasema kiungo wa Simba, Amri
Kiemba amesajiliwa na Yanga tayari kwa kuitumikia timu hiyo kwa msimu
ujao.
Akizungumza
na mtandao huu, mtu mmoja kutoka kamati ya usajili ya Yanga, amesema
Kiemba amesajiliwa kwa mkataba wa miaka miwili ili kuongoza nguvu katika
safu ya usajili ya Yanga.
Mtandao
huu unaahidi kuwasiliana na Kiemba muda mfupi atakapotoka mazoezini
katika kambi ya Taifa Stars kujiandaa na mechi ya kuwania kufuzu Kombe
la Dunia 2014.
Atakapotoka mazoezini mtandao huu utawasiliana naye kiungo huyo ili aweze kueleza ukweli juu ya usajili wake kwa Yanga.
Kiemba aliwahi kuichezea Yanga miaka ya nyuma kabla ya kutimka katika timu hiyo.
No comments:
Post a Comment