MTUHUMIWA
mmoja kati ya tisa waliotiwa mbaroni na jeshi la polisi baada ya
kutokea mlipuko wa bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi
amefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka 21 ya ma
uaji na kujaribu kuua.
Kesi
ya mshtakiwa Victor Ambrose Calist (20) ambaye ni dereva wa bodaboda na
mkazi wa eneo la Kwa Mromboo jijini Arushai amesomewa mashtaka yake
mbele ya Hakimu mkazi, Devotha Kamuzora.
Mtuhumiwa
huyo anakabiliwa na mashtaka matatu ya mauaji ya watu watatu
waliofariki dunia katika tukio ambalo lililotokea Mei 5, mwaka huu.
Mawakili
wa serikali, Haruna Matagane na Zachariah Elisaria wanadai Calist pia
anatuhumiwa kwa makosa 18 ya kujaribu kuua. Hata hivyo makosa mengine
bado hajatajwa mpaka hivi sasa.
Pia
polisi imewaachia huru raia wanne wa kigeni waliokuwa wakishikiliwa kwa
tuhuma za kuhusika katika tukio hilo baada ya uchunguzi uliofanywa na
jeshi hilo kwa kushirikiana na FBI na polisi wa kimataifa (Interpol),
kubaini hawakuhusika kurusha bomu katika kanisa
No comments:
Post a Comment