Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, May 23, 2013

BAADA YA LWAKATARE KUFUTIWA KESI YA UGAIDI, DPP AOMBA MAHAKAMA IFANYE MAREJEO YA KESI HIYO. SOMA ZAIDI HAPA


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj-qQ6BCowBsJ_au6pmmOIE5x0Lz2LAj1LycXCsPolzGUL8ecac95fBi7mJ5c-h9HEwPcN2Gm_6t9vCbS-rVXDbOy2uFAXawerVu_1XOSyNSUhXCTOsrAG33IGaxe6ygVfq3GhWWSxCmccK/s1600/Pg.1.JPGMKURUGENZI wa Mashitaka (DPP) amewasilisha maombi ya kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, uliomfutia mashitaka ya ugaidi Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare na mshitakiwa mwenzake Ludovick Joseph.
Katika ombi hilo lililowasilishwa juzi katika Mahakama ya Rufaa, DPP anaomba mahakama ifanye marejeo ya uamuzi huo na kuamuru kuwa haukuwa sahihi kisheria. Mei 8 mwaka huu, Jaji Lawrence Kaduri alifuta mashitaka matatu ya ugaidi dhidi ya washitakiwa hao kwa kuwa hati ya mashitaka iliyofunguliwa na DPP, haielezi uhalisia wa kosa hilo na washitakiwa wanahusika vipi kufanya ugaidi.
Katika ombi hilo, Mkurugenzi Mashitaka anaiomba mahakama hiyo iite na kuangalia rekodi za Mahakama Kuu kwa nia ya kujiridhisha usahihi, uhalali wa uamuzi huo pamoja na amri zilizotolewa.
Aidha anaomba mahakama kufuta uamuzi kuhusu uhalali wa mashitaka wanayodai yalikuwa ya awali, ione kuwa walalamikiwa walikuwa hawajaitwa kujibu mashitaka yao, pia haikuwa sahihi kwa mahakama hiyo kuamua kuhusu uhalali huo.
Anaomba mahakama ione kwenye sababu zilizoombwa na walalamikiwa katika ombi lao, hakuna ombi la kufuta mashitaka dhidi yao, pia hakuna taarifa zilizowasilishwa na walalamikiwa ambazo Mahakama Kuu ingeamua uhalali wa mashitaka au kuwepo kwa mapungufu.
DPP anaomba mahakama iamuru kuwa uamuzi wa Mahakama Kuu, kufuta baadhi ya mashitaka kwenye hati ya mashitaka ya muda haukuwa sahihi kisheria.
Machi 22 mwaka huu, Lwakatare kupitia kwa mawakili wake aliwasilisha ombi la kutaka mahakama hiyo ifanye marejeo ya mwenendo wa kesi ya ugaidi, inayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya DPP kufuta mashitaka dhidi yao, kisha kuwakamata na kuwasomea upya.
Washitakiwa hao walifutiwa mashitaka ya kupanga njama za kufanya kitendo cha ugaidi cha kumteka Mhariri wa gazeti la Mwananchi, Dennis Msacky kupanga na kushiriki mkutano wenye lengo la kutenda kitendo cha ugaidi ambacho ni kumteka Msacky.
Lwakatare alifutiwa mashitaka ya kuruhusu mkutano kati yake na Joseph, kufanyika nyumbani kwake katika eneo la King’ongo, Kimara Stop Over, kwa lengo la kuhamasisha vitendo vya ugaidi.
Kutokana na uamuzi huo, sasa washitakiwa hao wanadaiwa Desemba 28 mwaka jana katika eneo la King’ongo, Kinondoni, Dar es Salaam walipanga njama ya kutenda kosa la jinai la kutumia sumu kumdhuru Msacky. Shitaka hilo lina dhamana.
CHANZO : HABARI LEO

No comments:

Post a Comment