Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, May 30, 2013

BENKI YA DUNIA NA DANIDA KUWEZESHA MAMLAKA KUPITIA MRADI WA UENDELEZAJI MIJI(TSCP),TANZANIA STRATEGIC CITIES PROJECT


Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, 
Kaimu katibu mkuu, ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Bw. Jumanne Sagini(Kushoto) akikagua ujenzi wa daraja , eneo la Mwangaza –Kisasa mjini Dodoma. Wengine ni wawakilishi wa mradi wa uendelezaji miji Tanzania (TSCP)SONY DSC 
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI, Mhe Aggrey Mwanri, (kati) akitoa maoni yake kuhusu ujenzi wa stendi ya mabasi Jamatini kwa timu ya Benki ya Dunia na Ubalozi wa Denmark, na wengine ni wawakilishi wa mradi wa uendelezaji miji Tanzania (TSCP) na wawakilishi kutoka serikali saba za Mitaa na mamlaka ya maendeleo wakati wanatembelea maeneo husika, ambayo ilikuwa ni sehemu ya kongamano ya kutathmini maendeleo ya TSCP  iliyofanyika Mei, 2013.
Benki ya Dunia yatoa mikopo kwa ajili ya kutekeleza mradi wa kuendeleza miji ujulikanao kama “Tanzania Strategic Cities Project” (TSCP) ambao umeundwa kwa ajili ya kukabiliana na changamoto mbalimbali nchini Tanzania zikiwemo kasi kubwa ya ongezeko la watu, miundombinu isiyokidhi mahitaji ya Miji husika na kutokuwa na rasilimali fedha kwa ajili ya kusimamia miundombinu na huduma nyingine za kijamii.

No comments:

Post a Comment