Habari zilizopo hivi sasa kutoka Ruaha wilaya ya Kilosa mkoani Moro ni
kwamba kuna mapambano yanaendelea hivi sasa kati ya raia na askari wa
kutuliza ghasia ambao wanatawanya raia kwa mabomu ya machozi. Imeelezwa
na ripota wetu kutoka Ruaha kuwa chanzo cha mapambano hayo ni mvutano
ulioibuka kati ya Wanakijiji na Serikali ya kijiji cha Ruaha, baada ya
wanakikiji kuutaka uongozi uachie ngazi na uongozi kugoma kuachia ngazi.
Imeelezwa zaidi kuwa kufuatia hali hiyo, wanakijiji walivamia ofisi za
serikali ya kijiji na kukiteka hali iliyowalazimu askari kuitwa ili
kutawanya raia. Hali haikuwa rahisi, kwani raia waligoma kutawanyika
na askari wakalazimika kufyatua mabomu ya machozi ambayo yalipigwa
mpaka yakaisha lakini raia wakawa bado wapo, askari walilazimika kufuata
mengine na hali bado ni tete hadi muda huu.
No comments:
Post a Comment