Pages

Wednesday, May 22, 2013

BreakingNewss: Nyumba ya mwandishi wa TBC, CCM Yachomwa moto huku mabomu na risasi zikirindima

 
Hali Mtwara bado ni tete: ITV wameripoti muda si mrefu kuwa jengo la CCM Wilaya ya Mtwara limeteketezwa kwa moto, baada ya kupigwa kiberiti na watu wasiojulikana.
Hali imezidi kuwa mbaya katika Mji wa Mtwara na hivi punde watu wanaendelea kufanya uharibifu katika maeneo mbalimbali ya mji huo.Jengo moja ambalo linadaiwa kumilikuwa na CCM limechomwa moto katika eneo la Majengo na daraja linalounganisha Lindi na Mtwara limevunjwa.Mbali na hayo pia nyumba ya mwandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC)
imechomwa moto.Katika Mji wa Mtwara milio ya mabomu na risasi ndio inayosikika kila kona. Jeshi la Polisi linajaribu kuwadhibiti vijana  na watu wengine ambao wanafanya vurugu hizo.

No comments:

Post a Comment