WAZIRI KAWAMBWA.WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI WAKIWA DARASANI.
RASIMU ya
Sera ya Elimu na Mafunzo nchini inapendekeza kuunganisha elimu ya
msingi na sekondari ya kawaida ya sasa ili kuunda elimu-msingi
itakayotolewa kwa kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2018, imefahamika.
Rasimu ya
kwanza ya Sera hiyo imeshakamilika na sasa wadau mbalimbali wanatoa
mapendekezo yao kuiboresha, kabla ya kupelekwa bungeni ili kutungiwa
sheria.
Aidha,
mikakati hiyo itakayotekelezwa ni kuhuisha muundo na utaratibu mpya wa
elimu na mafunzo kwa kuhakikisha kila mtoto mwenye umri wa miaka mitatu
na mitano anapitia elimu ya awali kwa kipindi kisichop
Naibu
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo alithibitisha kwa
gazeti hili wiki hii mjini hapa kuhusu kukamilika kwa rasimu ya kwanza
ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2013.
“Ni kweli
Sera hiyo imekamilika baada ya kuandaliwa kwa miaka mitatu. Imepita kwa
wadau mbalimbali, mashuleni, vyuoni na katika taasisi mbalimbali nchini
ambao wametoa maoni yao.
“Jumapili
(kesho) tunatarajia kuwa waheshimiwa wabunge nao watapata fursa ya
kuijadili na kutoa maoni yao katika semina iliyoandaliwa maalumu kwao,”
alisema Mulugo katika Viwanja vya Bunge.
No comments:
Post a Comment