KIJANA
mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja anayedaiwa ni
mzoefu wa wizi kwa kutumia usafiri wa pikipiki ‘bodaboda’, ameuawa baada
ya kumliza mwanamke aliyetambulika kwa jina la Jusmini.
Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa
wiki iliyopita maeneo ya Mwenge jijini Dar, saa tatu usiku ambapo
inadaiwa mwanamke huyo alikuwa akikatiza mitaa hiyo huku akiwa ameweka
mkoba wake kwapani.
Ikadaiwa mwanamke huyo akiwa eneo
hilo huku akiamini yuko salama, ilitokea bodaboda kwa nyuma ikiwa
imebeba abiria na ghafla alishangaa anakwapuliwa mkoba wake.
“Unajua yule mama alikuwa
akitembea kwa kujiamini lakini inavyoonekana wale jamaa ambao ndiyo zao
kuwaibia watu walikuwa wamemlia ‘timing’ tangu aliposhuka kwenye
daladala.
“Tuliposikia makelele ya mwizi,
tulimfuata mama huyo na tulipomuuliza akatuambia ameibiwa mkoba wake
huku akituonesha vijana hao ambao muda huo walikuwa wakikimbia,”
kilieleza chanzo hicho kilichoshuhudia tukio zima.
Ikaelezwa
kuwa, kufuatia maelezo ya mwanamke huyo, baadhi ya watu wenye hasira
kali wengine wakiwa kwenye pikipiki waliamua kuwakimbiza wezi hao ambapo
mmoja alishuka na kukimbia kivyake huku mwenye bodaboda akizuiwa kwenye
geti kuu ya kutokea magari.
“Alipozuiwa
akaona imeshakua soo, akashuka na kuitelekeza pikipiki yake kisha
akataka kudandia gari nyingine lakini watu wakafanikiwa kumkamata kwenye
mataa ya Mwenge ambapo magari yalisimama, jamaa alishushiwa kichapo
hadi akauawa,” kiliendelea kupasha chanzo hicho.
Baada
ya kijana huyo kuuawa, polisi walifika eneo la tukio na kuuchukua mwili
wake. Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Charles Kenyela
(pichani)alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo alisema taarifa za kifo cha
kijana huyo hazijafika mezani kwake lakini akasema anaendelea kufuatilia.
No comments:
Post a Comment