ANTiVIRUS DAWA YA Virus WA Hiphop in Tanzania
WARAKA NAMBA 1(ZIPO 88) KILA WIKI UTAPATA WARAKA MMOJA
Ni wazi na dhahiri kabisa kesi
iliofunguliwa mahakamani dhidi ya Lady JayDee haina maana yoyote
isipokuwa ni hofu ya mafisadi wa muziki nchini (Kusaga na Ruge) kwa kuwa
waraka wa pili ulikuwa utoke tar 15 may na mwingine tar 17 may mwaka
huu wa 2013.
Hapa la kujiuliza ni juu ya interview
ya Rugen a kinachoendelea sasa,eti suala limefika mahakamani,kweli
Kusaga na Ruge mmeweza kuthibitisha nyie ni mafisadi na mnamuaibisha
Rais Kikwete ambaye nina uhakika anajua kuwa nyie ndio kikwazo kikubwa
na hata Bungeni alishawahi kuzungumza kuwa alitoa studio na pango kumbe
tatizo sio hilo,tujiulize wote kuna nini wanachoficha hadi kumtafutia
kesi raia mwema asie na hatia?
Tena anaejitafutia rizki ambayo wao wanapigana nayo kwa kumkandamiza?
Huku wakitumia mabavu wakilindwa na
baadhi ya viongozi wa serikali na waandishi ambao majina yao mtayapata
kupitia nyaraka zinazokuja (zipo 88) na huu ndio wa kwanza.
Nimesikitika sana na njia pekee ya
kuufahamisha umma juu ya ufisadi huu wa Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga
ni kuyaanika yote ambayo jamii na Viongozi wa Serikali kama mlikuwa
hamjui sasa ndio wakati muafaka wa kuwajua watu hawa ambao kila kukicha
ni kuimarisha ufisadi wao na kujipendekeza kwa Viongozi sambamba na
watoto wao (mtajua mpaka majina yao)
Naanza kupatwa na wasiwasi
nikijiuliza, endapo Lady JD angekuwa amegombana na msanii mwenzake
mkubwa kama Prof Jay, Ray C au Juma Nature wanasiasa wangeingilia kati?
Ni wazi wasingesogea kwa kuwa hakuna maslahi zaidi ya kuingilia mgogoro
huu ambao hawataki jamii ijue maovu yao.
Napatwa mashaka jinsi wanasiasa wanavyolivalia njunga jambo binafsi
Kama hili na kulifanya ni la
kiserikali basi tafuteni chanzo cha tatizo mjue ni sehemu gani sahihi ya
kuanza kutatua kilichopo na sio kukimbilia kuunda vikao ambavyo naamini
vimeshaitishwa vingi sana lakini hakuna kilichosaidia.
Wanasiasa badala ya kutafuta sababu
zinazofanya wasanii wanalalamika mnakimbilia kutatua mgogoro wa Ruge na
JD ili kusuluhisha mambo yasiendelee kuongelewa jamii ijue uovu wa
mafisadi hawa.
Haitasaidia kwa sababu wanaojua maovu
ya hawa mafisadi Rugen na Kusaga ni wasanii wengi wakubwa na watu
wengine binafsi (kumbukeni waraka zipo 88)
Vijana mnaowategemea katika kampeni
zenu na mnawaita Taifa la kesho, lakini mnakubali waendelee kukandamizwa
na kunyanyasika huku wakizidi kuwaneemesha kina Ruge na Kusaga.
Tatizo mnalijua kaeni na wasanii wote
wawaelezee matatizo yao, msikae na wasanii ambao wanaamrishwa na kina
Ruge. Sikilizeni kilio cha wasanii wengine pia na itafutwe njia ya
kupata maoni ya kila mmoja na kuachana na watu wengine ambao wanaendesha
mtandao wa ufisadi chini ya kivuli cha Ruge (Said Fella na Babu Tale)
ambao mtapata kujua kila kitu kuhusu ufisadi wao na kinachoendelea
(kumbuka waraka zipo 88)
Ruge Mutahaba amekuwa ni tatizo na
janga la Kitaifa katika tasnia ya muziki kwa ujumla, amekuwa akiwagawa
wasanii kwa kutumia redio Clouds kwa vitisho vya kutopigiwa nyimbo, au
kwa danganyio la kufanyiwa promotion mpaka kwenye magazeti endapo tu
utakuwa chini ya bawa lake.
Wasanii wamekuwa hawalipwi vizuri ili waendelee kumtegemea fisadi huyu.
Kwani wasanii wote wangekuwa na
kipato cha kuweza kusimama imara leo hii kauli kama ya Lady JD
ingezungumzwa karibu na kila mwanabongoflava.
Fred Kavishe (fisadi mwingine) ambae
anasimamia Kili music awards yuko bega kwa bega na Ruge kudanganya
wananchi nani ni bora katika tuzo hizo ili kulinda maslahi yao binafsi.
Na wao huchagua wale wasanii ambao
hawana sauti za kudai haki yao ili wawatumie kadri wanavyotaka.Tuzo za
Kili ni uozo mtupu.Imefikia wakati basata itoe vibali kwa wadau wengine
wa muziki (nako kuna ufisadi)wasio na interest binafsi na wasanii wao,
kuendesha hizi shughuli ili kukuza muziki.Kutokuwepo na tuzo zingine
kunasababisha ionekane kuwa basata nao wamo kwenye mgao wa mabepari hao
wanaoua sanaa ya Tanzania
JINSI RUGE NA KUSAGA WANAVYOTAWALA
Njia anayoitumia Ruge na Kusaga iko
wazi, wao wana redio na hapo hapo wana wasanii wao.Hivyo promotion
inabidi wafanyie wasanii wao ambao ni waoga ili waweze kuwatumia bila
wasanii hao kufanya fyoko fyoko.
Wasanii wengine ambao sio chini ya
Clouds kwa kuwa hawana jinsi nyingine ya kupata hela inabidi
wainyenyekee Clouds wakiamini ndio njia pekee ya kuwapatia vipato
Huku wakisubiri show moja ya fiesta ya kila mwaka.
Huko katika fiesta kuna wengine
wanalipwa mpaka laki tatu na bado katika hiyo ili upangwe kwenye list ya
kupanda jukwaani B12 nae lazima akate laki moja yake.
Hapo msanii anabakiwa na nini akirudi nyumbani?
Hivi laki tatu ni nini kwa maisha ya msanii?
Njia pekee ya kuwatawala ni kuwafanya waendelee kuwa maskini.
Leo hii mtangazaji wa redio ana sauti kuliko msanii.
Kwanini redio zingine hazilaumiwi? Ni
kwa sababu hazijihusishi moja kwa moja na wasanii.Hilo ni kosa kubwa
sana linalofanywa na Clouds au pengine ndio mtazamo wao walioamua
kuufuata kwa sababu wanaamini Serikali ipo mikononi mwao.
Maisha na ajira za watoto wa watu ambao wengi hawajasoma wanategemea vipaji, mnayakatili bila huruma
Mwisho tumuombee Lady JD Mahakama
imruhusu azungumze yote, kila mtu anataka kusikia sio siri Clouds, Ruge
na Kusaga ni nyonya damu.
Mahakama itambue kuwa wanaojua maovu
ya Rugen a Kusaga sio Lady JayDee pekee ni wengi mno na kama njia ya
kukimbilia mahakamani ndio wameichagua basi ongezeni mahakama kwa kuwa
tupo wengi tutakuja kuyaongea kuhusu mafisadi hawa wa Clouds (siku hizi
wanaitwa wafu)
Hela ina nguvu hata palipo na haki,
JD hajatukana matusi na amekuwa makini katika kutoa kauli zake sasa
anashitakiwa kwa kosa gani? Anashitakiwa kwa kudai haki yake. Anaconda
wewe songa na sisi tunakuja kizimbani na sasa ndio TANZANIA itawajua
Rugen a Kusaga ni kina nani na walianzia wapi,walikuwa wapi,wako wapi na
nani wanaoshirikiana nao,JIPANGENI!
SAIDIA KUSAMBAZA NENO..
MDAU
No comments:
Post a Comment