Na Tamimu Adam- Jeshi la Polisi
Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema amewavisha vyeo maofisa
waandamizi wa Jeshi la Polisi 21 katika hafla fupi iliyofanyika Makao
Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es salaam. IGP Mwema aliwavisha
maofisa hao vyeo hivyo baada ya kupandishwa na mheshimiwa Rais na
Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuanzia mei 28 mwaka huu.
Katika
hafla hiyo, IGP Mwema aliwavisha maofisa wawili cheo cha Kamishina wa
Polisi ambao walipandishwa kutoka cheo cha Naibu Kamishina wa Polisi
(DCP) na kuwa kamishina wa Polisi(CP), maofisa hao ni aliyekuwa Naibu
kamishina wa Polisi Suleimani kova na Naibu Kamishina wa Polisi Issaya
Mngulu ambao sasa hivi wamepanda na kuwa makamishina wa Polisi.
Wengine
19, walivishwa vyeo vya Naibu Kamishina wa Polisi ambao nao pia
walipandishwa kutoka cheo cha kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi na
kuwa Naibu kamishina wa Polisi ni Pamoja na Mkuu wa utawala na
rasilimali Naibu kamishina wa Polisi(DCP) Thobias Andengenye, Mkuu wa
Opereheni Naibu Kamishina wa Polisi (DCP) Simon Sirro, DCP Brown Lekey,
DCP Hamdani Omari Makame, DCP Kenneth Kasseke, DCP Sospeter Kondela, DCP
Ernest Mangu, DCP Abdulrahman Kaniki, DCP Adrian Magayane, DCP Husseni
Laisseri, na DCP Anthon Mwami.
Wengine
kati yao ni DCP Mohamed Mpinga, DCP Mpinga Michael Gyumi, DCP Ally
Mlege, DCP Hezron Gyimbi , DCP Jonas Mugendi na DCP Michael Kamuhanda
ambaye ni kamanda wa polisi mkoa wa Iringa.
Miongoni
mwa maofisa waandamizi wa jeshi la polisi walipandishwa cheo cha Naibu
kamishina wa Polisi, wapo maofisa wawili(2) wa kike ambao ni alikuwa
Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Bi. Adolfina Chialo ambaye sasa
amepanda na kuwa Naibu Kamishina wa Polisi (DCP) na aliyekuwa Kamishina
Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Bi. Elice Mapunda naye pia amepanda na
kuwa Naibu Kamishina wa Polisi(DCP).
Kwa
upande wake Naibu kamishina wa Polisi (DCP) Elice Mapunda alisema kuwa
yeye ameshukuru sana kupata cheo hicho, kwani ni mara ya kwanza kwa
mofisa wa kike wa Jeshi la Polisi kupata cheo hicho katika Jeshi la
Polisi
IGP Mwema
alitumia nafasi hiyo kumshukuru Mheshimiwa rais na amiri Jeshi Mkuu wa
Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa
kutambua mchango wa utendaji wa maofisa wa Jeshi la Polisi katika
kuimarisha usalama wa raia na mali zao,
Aliongeza
kuwa “ Ni heshima kubwa sana kwa Jeshi la Polisi kusema kuwa
amelijengea Jeshi mpanuko mkubwa kwani tangu tupate uhuru mwaka 1961
hatujawahi kupanua jeshi kwa kiwango hiki.
Aliwataka
maofisa walipandishwa vyeo kuwa kioo na mfano katika kusimamia,
kupanga na kutathimini kwa kuonyesha dira ili maofisa na askari
wengine waweze kuiga katika kutoa huduma bora kwa ndani na nje.
No comments:
Post a Comment