Waombolezaji
katika msiba nchini Zimbabwe walipigwa na butwaa pale mtu aliyekufa
alipoamka wakati wakipita kando ya jeneza lake kutoa heshima za mwisho,
shirika la habari za nchi hiyo limeripoti jana.
Brighton
Dama Zanthe, mwenye miaka 34, aliingizwa ndani ya jeneza Jumatatu
iliyopita baada ya kuwa amefariki nyumbani kwake baada ya kuugua kwa
muda mrefu.
Familia
iliyojawa na huzuni ya mfanyakazi huyo wa usafirishaji ilifunika mwili
wake kwa mablanketi na kufanya mipango ya kumhamishia kwenye mochari ya
mjini humo, kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa katika gazeti la The
Herald.
Lakini siku iliyofuata marafiki wa
Zanthe na jamaa zake walisambaratika wakiwa hawaamini pale alipoanza
kutembea wakati wakipita mbele ya jeneza kuaga mwili wa 'marehemu' huyo.
Bosi wa 'marehemu' huyo, Lot Gaka alieleza kuhusu mkasa huo alipobaini mfanyakazi wake alikuwa bado angali hai.
Alisema: "Kwanza niligundua miguu
ya Zanthe ikisogea wakati nilipokuwa kwenye ya foleni kutazama mwili
wake. Hili lilinishitua mno. Kwanza sikuweza kuamini macho yangu lakini
baadaye nilibaini kwamba kulikuwa na kusogea kwa viungo kadhaa katika
mwili wake huku waombolezaji wengine wakiwa hawaamini kinachoendelea."
Gaka, ambaye anaendesha kampuni ya
mabasi katika mji wa Gweru, alisema Zanthe alikuwa hana afya njema
kabla ya 'kifo' chake wiki iliyopita.
Alielezea minsi alivyotembelea
nyumbani kwa familia hiyo kutoa msaada pale mke wa mfanyakazi wake
alivyompigia simu kumweleza kwamba Zanthe alikuwa amefariki.
Alisema: "Zanthe alikuwa katika
likizo ya ugonjwa kwa kipindi fulani na kila mmoja kazini alikuwa
akifahamu kwamba hali yake ilikuwa mbaya.
"Tulimtembelea nyumbani kwake.
"Sikushangaa pale nilipopokea simu
kutoka kwa mke wa Zanthe Jumatatu usiku wiki iliyopita akisema kwamba
mume wake alikuwa amefariki."
Aliongeza: "Nilitembelea maduka
mawili yanayouza majeneza mjini humo kwa ajili ya kuulizia gharama kabla
ya kuelekea nyumbani kwa Zanthe hivyo kuweza kuchukua mwili wake na
kuuhifadhi katika mochari.
No comments:
Post a Comment