Mbunge, Naibu Waziri watajwa mauaji ya kamanda Liberatus Barlow! Shuhuda ahifadhiwa kwa IGP Mwema...
- Kijana Mohamed Malele aliyejisalimisha kwenye vyombo vya ulinzi na
usalama akijitambulisha kuwa mshirika wa mtandao uliohusika kumuua
kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, amepewa
hifadhi maalum na IGP wa polisi Said Mwema. Kutokana na sababu za
kiusalama, tunalinahifadhi jina la mtaa alikohifadhiwa!
Kijana Mohamed Malele aliyejisalimisha kwenye vyombo vya ulinzi na
usalama akijitambulisha kuwa mshirika wa mtandao uliohusika kumuua
kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, amepewa
hifadhi maalum na IGP wa polisi Said Mwema.
Jamhuri imenasa taarifa kwamba malele anahifadhiwa ktk nyumba maalum
jijini Dar es Salaa akilindwa na polisi wenye silaha na kupewa huduma
zote za kibinadamu. Kutokana na sababu za kiusalama gazeti hili
linahifadhi jina la mtaa alikohifadhiwa.
Malele ana siri nzito juu ya mtandao mpana wa mauaji ndani ya jeshi la
polisi unaohusisha watumishi wengine kutoka vyombo vya ulinzi na
usalama, wafanya biashara na wanasiasa.
Habari za karibuni kabisa zinasema kwenye mtandao wa uhalifu wamo
wabunge na naibu waziri. Jamhuri linaendelea kuhifadhi majina yao kwa
kuwa haijafanikiwa kuzungumza nao.
Mtandao huo unatajwa na malele ambaye ni mkazi wa kijiji cha Igoma,
Kwimba Mwanza, kuwa ndio uliohusika na mauaji ya kamanda Barlow usiku wa
kuamkia octoba 13 mwaka jana ktk eneo la Kitangiri jijini mwanza,
alipokuwa anamrejesha mwalimu anayetajwa kwa jina la Doroth Moses,
aliyekuwa naye ktk kikao cha harusi.
Malele alikamatwa ijumaa may 10, mwaka huu alipokuwa ktk Lango la Bunge mjini Dodoma wakati akitafuta wabunge kadhaa.
Malele anatajwa kuwa mtu muhimu ambaye taarifa zake zinawasaidia
viongozi wa juu wa vyombo vya ulinzi na usalama na serikali kwa ujumla
kutambua na kuufumua mtandao wa uhalifu ndani ya Jeshi la
polisi................... habari zinaedelea japo nyingi ni paraphrase ya
taarifa za gazeti hilo hilo za wiki iliyopita.
source jamii forum na gazeti la jamhuri
link iyo https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/458632-mbunge-naibu-waziri-watajwa-mauaji-ya-kamanda-liberatus-barlow-shuhuda-ahifadhiwa-kwa-igp-mwema.html
No comments:
Post a Comment