li
Mchezo ulisimama kwa muda sababu ya ubaguzi
Balotell
Balotelli na Kevin Prince-Boateng wakiwa wamesimama pamoja wakati wa tangazo linatolewa uwanjani
Sulley Muntari alitolewa nje kwa kumsihi refa
MECHI ya
AC Milan ya Serie A usikuwa jana ilisimama kwa muda kwa sababu kejeli za
kibaguzi ambazo zilielekezwa kwa Mario Balotelli na wachezaji wengine
weusi kutoka kwa mashabiki wa Roma.
Refa
Gianluca Rocchi alisimamisha mechi na mtangazaji wa uwanjani akawaambia
mashabiki wa Roma waache kuwafanyia ishara za nyani wachezaji weusi wa
Milan, vinginevyo mechi itaahirishwa.
Mapema
Sulley Muntari alitolewa nje kwa kadi nyekundu wakati anakwenda kumsihi
refa huyo aliyeonekana aataka kumpa kadi ya pili ya njano Balotelli.
Massimo Ambrosini alikuwa miongoni mwa wachezaji waliokwenda kulalamika kwa refa Rocchi kabla ya mechi kusimamishwa.
Totti
baadaye alitolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu beki wa
Milan, Phillipe Mexes na mechi hiyo ikaisha kwa sare ya bila kufungana.
Mchezo wa
kirafiki Januari baina ya Milan na Pro Patria ulisimamishwa pia kwa
sababu kejeli za kibaguzi alizofanyiwa Kevin-Prince Boateng.
Shirikisho
la soka Italia limeweka sheria mpya kuwasaidia marefa kudhibiti ubaguzi
baada ya kiungo wa Milan, Kevin-Prince Boateng kuamua kuondoka uwanjani
January katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Pro Patria baada ya kukutana
na dhalili hiyo.
No comments:
Post a Comment