Kwaheri: Neymar alikuwa mpweke kabla ya kuichezea Santos mechi ya mwisho
MSHAMBULIAJI
Neymar alimwaga machozi usiku wa kuamkia leo, wakati akiichezea klabu
yake, Santos mechi ya mwisho kabla ya kuhamia Barcelona.
Nyota
huyo wa Brazil atakayejiunga na vigogo hao wa Catalan kwa mkataba wa
miaka mitano msimu ujao aliiaga klabu yake iliyomlea kisoka kwa sare ya
0-0 na Flamengo.
Katika
taarifa yake aliyotoa jana kwenye Instagram, alifafanua ni kiasi gani
hatawasahu mashabiki wa Santos ambayo iko moyoni mwake.
Neymar
aliandika: "Nataka kuwashukuru mashabiki wa Santos kwa miaka tisa
mizuri. Hisia zangu kwa klabu na mashabiki hazitabadilika!
"Ni klabu
kama Santos FC pekee inaweza kunipa kila kitu nilichojifunza ndani na
nje ya Uwanja. Nawashukuru mashabiki baab kubwa, ambao wamenisapoti hata
katika wakati mgumu.
"Mataji, mabao, chenga, ushangiliaji na nyimbo mashabiki walizotunga kwa ajili yangu vitadumu daima moyoni mwangu...'
WASIFU WA NEYMAR
1992: Februari 5 - Alizaliwa mjini Mogi das Cruzes, Brazil.
2003: Alijiunga na akademi ya Santos.
2006: Alikwenda Hispania kufanya majaribio Real Madrid, lakini akaamua kubaki Santos.
2009: Machi - Aliichezea mechi ya kwanza
Santos akiwa na umri wa miaka 17 kabla ya kuifungia bao lake la kwanza
timu ya wakubwa wiki moja baadaye.
2010: Aprili 15 - Alifunga mabao matano Santos ikiifunga Guarani 8-1.
Mei - Aliteuliwa Mchezaji Bora wa Campeonato Paulista huku Santos ikishinda taji.
Julai - Mkurugenzi wa Soka wa Santos, Pedro
Luiz Nunes alisema klabu ilikataa ofa ya Pauni Milioni 12 kutoka West
Ham. Neymar pia alikanusha amekubali kujiunga na Chelsea.
Agosti 10 - Alifunga bao akiichezea Brazil
kwa mara ya kwanza ikiibuka na ushindi wa 2-0 katika mchezo wa kirafiki
dhidi ya Marekani.
Desemba 30 - Alikuwa wa tatu katika kura za
uteuzi wa Mwanasoka Bora wa Mwaka Amerika Kusini, baada ya kufunga
mabao 42 katika mechi 60.
2011: Juni - Alifunga wakati Santos ikitwaa
taji la Copa Libertadores kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1963 - wakati
Pele bado anaichezea klabu hiyo.
Novemba - Alisaini mkataba mpya na Santos kuendelea kuichezea hadi baada ya Kombe la Dunia 2014 Brazil.
Desemba - Aliteuliwa kuwania tuzo ya
Mwanasoka Bora wa Dunia wa FIFA na akashinda tuzo ya Puskas kutokana na
bao lake dhidi ya Flamengo.
Alishinda Medali ya Shaba katika Klabu Bingwa ya Dunia, Santos ikifungwa na Barcelona 4-0 katika Fainali.
Desemba 30 - Alishinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka Amerika Kusini.
2012: Februari 5 - Alifunga bao lake la 100
katika timu ya wakubwa, akisherehekea kutimiza miaka 20 ya kuzaliwa
katika mechi dhidi ya Palmeiras.
Mei - Alifunga mabao mawili kwa miguu yote kwenye Fainali ya Campeonato dhidi ya Guarani, Santos ikishinda 7-2 jumla.
Juni- Aliibuka mfungaji bora wa Copa Libertadores, lakini Santos ilifungwa katika Nusu Fainali na Corinthians.
Desemba - Alishinda tuzo ya Mwanasoka Bora
wa Mwaka wa Amerika Kusini kwa mara ya pili, wakati pia alishinda Kiatu
cha Dhahabu kama mchezaji bora katika michuano ya ubingwa wa Brazil.
Alikanusha kuwa na mpango na Barcelona.
2013: Machi 18 - Alisema kucheza Ulaya ni ndoto yake.
Aprili 25 - Baba yake na wakala wake, Neymar da Silva Sr, alisema Neymar ataondoka Santos kabla ya Kombe la Dunia mwakani, 2014.
Mei 25 - Santos ilitangaza kukubali ofa mbili kwa ajili ya mshambuliaji huyo, moja ya Real Madrid na nyingine Barcelona.
Mei 26 - Neymar na Barcelona wanathibitisha amechagua kujiunga na mabingwa hao wa Hispania.
No comments:
Post a Comment