Pages

Saturday, May 4, 2013

MFANYA BIASHARA ALIYEJIRUSHA TOKA GOROFA YA TISA AFARIKI DUNIA


Mfanyabiashara Costa Shrima Aliyejirusha toka ghorofa ya 9 ya Hoteli ya Concord iliopo Maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam alifariki  jana muda mfupi baada ya tukio hilo.
Mfanya biashara huyu mkazi wa Dar es salaam mzaliwa wa Moshi kilimanjaro alikutwa na mauti hayo baada ya kujirusha kutoka gorofa ya tisa ya hoteli hiyo ambayo alienda kwa lengo la kuuona ukumbi wa tukio hilo ambao uko gorofa ya tisa ya hoteli hiyo.
Chanzo Cha Mfanyabiashara huyu kujirusha bado hakijafahamika mpaka sasa.
Taratibu za Mazishi ya Marehemu Zinapangwa jijini dar es salaam  na tukizipata tutakuhabarisha mapema. 
Ndugu Costa shirima ameacha mke na watoto.
Mungu ailaze roho ya marehemu Mahali Pema Peponi 
Amina

No comments:

Post a Comment