YULE
mfanyabiashara wa jijini Dar ambaye hivi karibuni alifumaniwa gesti
akiwa na mwanafunzi wa kidato cha pili, huenda akapandishwa kizimbani
siku yoyote.....
Kwa mujibu wa dada wa mwanafunzi
huyo ambaye aliomba jina lake lisiandikwe , baada ya mfanyabiashara
huyo kufumaniwa na binti huyo mwenye umri wa miaka 16, aliahidi kutoa
fedha za Kimarekani dola 400 (zaidi ya Sh. 640,000) kama faini kwa
kitendo hicho.
Hata hivyo, pamoja na kukubali kutoa kiasi hicho, mfanyabishara huyo hakutimiza ahadi yake na kuamua kuingia mitini.
Dada wa mwanafunzi huyo amedai
kuwa mfanyabiashara huyo anasakwa ili wamburuze mahakamani kutokana na
mwisho wa mwezi uliopita kushindwa kutimiza ahadi yake
No comments:
Post a Comment