Pages

Friday, May 3, 2013

MFANYABIASHARA KARIAKOO AJIRUSHA TOKA GHOROFA YA TISA NA KUANGUKIA GARI TAZAMA PICHA



Muda si mrefu huyu kaka kajirusha toka ghorofa ya 9 concord hotel kariakoo akaangukia kwenye hiyo taxi chanzo hata hakijulikani kapatwa na nini, ni mfanya biashara anaitwa Shirima kakimbizwa hosp.


Muda mfupi uliopita,Mtu mmoja alietambulika kwa jina la Shirima ambaye ni Mfanyabiashara katika moja ya Maduka ya Kariakoo jijini Dar es Salaam,amejirusha toka ghorofa ya 9 ya Hoteli ya Concord iliopo Maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam na amekimbizwa hospitali kwa uangalizi zaidi maana haijafahamika kama kapoteza Maisha au bado yu hai.

Mfanyabiashara huyo alijirusha toka ghorofani na kuangukia Gari aina ya Toyota Corolla ambayo ni taxi iliyokuwa imepaki nje ya hoteli hiyo....chanzo cha kujirusha kwa mfanyabiashara huyo bado hakijafahamika mpaka sasa.

Mashuhuda wa tukio hilo lililotokea muda mfupi uliopita,wanaeleza kuwa walipatwa na mshuko baada ya kusikika kishindo cha kitu kilichokuwa kimeangukia gari hilo na waliposogea kushuhudia ndipo walipobaini kuwa alikuwa ni mtu huyo alietambulika kwa jina moja la Shirima.

No comments:

Post a Comment