JESHI la
polisi limekumbwa na kashfa nyingine baada ya askari wake kudaiwa
kumpiga risasi msichana wa miaka 16 baada ya kumkuta akivunja amri ya
sita ndani ya gari.
(Jina
tunalihifadhi) alikumbana na mkasa huo Jumatano usiku eneo la Mbagala
Zakhem jijini Dar es Salaam, ambapo alipigwa risasi sehemu ya makalio
wakati akijaribu kuwakimbia polisi kwa kutumia gari la mpenzi wake.Mpenzi huyo (jina linahifadhiwa), alikamatwa na kuwekwa mahabusu na kufunguliwa kesi ya ubakaji.
Akizungumza
na NIPASHE Jumapili jana katika wodi ya Hospitali ya Temeke alikolazwa,
msichana huyo alisema siku ya tukio alikutana na kijana huyo majira ya
saa 8:00 usiku katika baa moja inayoitwa Kindau na kukubaliana kwenda
kushiriki tendo la ndoa kwa malipo ya Sh 20,000.
Alisema kutokana na muda huo kuwa usiku sana hawakuweza kwenda katika nyumba ya kulala wageni na badala yake walikwenda eneo la Zakhem na kisha walipaki gari kwenye uchochoro na baadae walianza kubanjua amri ya sita.
Wakiwa kwenye kilele cha mapenzi yao, ghafla walishtukia gari la polisi likiwajia kwa kasi kwa nia ya kuwakamata.
Alisema kutokana na muda huo kuwa usiku sana hawakuweza kwenda katika nyumba ya kulala wageni na badala yake walikwenda eneo la Zakhem na kisha walipaki gari kwenye uchochoro na baadae walianza kubanjua amri ya sita.
Wakiwa kwenye kilele cha mapenzi yao, ghafla walishtukia gari la polisi likiwajia kwa kasi kwa nia ya kuwakamata.
“Tuliagana
anilipe elfu ishirini wala hakunibaka kama anavyodai, wao polisi
walitukuta tayari tunamaliza lakini kutokana na woga tulikimbia ili
tusikamatwe,” alisema msichana huyo.
Alisema
wakati wanakimbia kwa kutumia gari la mpenzi wake askari mmoja alifyatua
risasi iliyopenya kwenye taa ya gari na kwenda kumjeruhi sehemu ya
makalio yake.
“Nilisikia mlio mkubwa wa bunduki, ghafla nilihisi kitu kimeingia mwilini mwangu na kuishiwa nguvu,” alisema kwa uchungu.
Alisema
kwa kuona hali hiyo, mpenzi wake alisimamisha gari kwa kujisalimisha na
polisi walipowafikia walimtaka mpenzi wake huyo atoe pesa kama malipo ya
kitendo chao cha kukutwa wakifanya mapenzi ama sivyo watampeleka
kituoni.
Alieleza
kuwa mpenzi wake hakuweza kutoa pesa hizo ndipo walipoamua kumpiga na
kumpeleka kituo cha polisi cha Mbagala na yeye alifikishwa hospitalini
hapo kwa ajili ya matibabu.
Hata
hivyo, ndugu na jamaa wa mpenzi wake wanapinga hatua ya polisi hao
kutumia nguvu kubwa kama watu hao walikuwa watuhumiwa wa ujambazi.
Wakizungumza
wakiwa kwenye kituo cha Polisi cha Mbagala kufuatilia hatma ya ndugu
yao, ndugu hao ambao hawakutaka majina yao yatajwe gazetini walisema
hatua ya polisi kupiga risasi huku wakitambua watu hao sio majambazi ni
kitendo cha kinyama.
“Tunachoshangaa
ni kwa nini polisi wapige risasi wakati wakijua hawakuwa majambazi ila
walikuwa wakifanya mapenzi, hata hilo jalada la kesi walilofungua
wanataka kuficha maovu yao na sio vinginevyo,” alisema ndugu mmoja
ambaye alijitambulisha kuwa shemeji yake.
Alisema
kimsingi tukio hilo lilikwenda katika makubaliano yao na sio ubakaji
kama wanavyodai, ila kinachofanyika kwa sasa ni kutaka kumlinda askari
mwenzao aliyejeruhi kwa risasi.
Kamanda
wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, David Misime, alipopigiwa simu kuelezea
tukio hilo, alisema kwa sasa hawezi kulizungumza kwa kuwa yupo nje ya
Mkoa kikazi.
No comments:
Post a Comment