Ndugu yangu ukishangaa ya Mussa basi shangaa na ya Filauni, Methali
hiii methibitika Songea baada ya Mtoto Bahati Upendo mwenye siku 3 toka
azaliwe alipo wekwa na mama yake kwenye mfuko wa mbolea na kutumbukizwa
kwenye shimo, Ndani ya shimo hilo amekaa siku 6 bila kula wala kunywa
hadi alipo okotwa na wasamalia wema, Hivi sasa yuko Hospitali ya Mkoa wa
Ruvuma akiwa Salama Salimini Yeyote Mwenyenafasi ya kusaidia mtoto
huyu anaweza kwenda moja kwa moja Hospitali au wasiliana na namba
zifuatayo mchango utafwatwa 0755061588 au 0755 731 234.
Dawati la Police Wanawake Mkoa wa Ruvuma wakiwa na Wauguzi kuangalia
usalama wa Mtoto huyo aliye Tupwa. Kutoka kulia ni Muguzi Rukia Twahili
anaye fuata Devota Umbela na aliye mshika mtoto Mwenyekiti wa Mtandao wa
Police Wanawake Fadhila Chacha na wa mwisho kushoto ni A nna Chaima
SOURCE demashonews.blogspot.com
No comments:
Post a Comment