Pages

Sunday, May 26, 2013

"MWANAMKE MCHAWI ADONDOKEA KANISANI AKIWA NA BIBLIA MKONONI, WAUMINI WAHAHA, YEYE MWENYEWE ANENA MAZITO "...!!

Wakati Mtwara kukilipuka kwa vurugu za gesi na kusababisha maafa, jijini Dar kumeibuka taharuki ya aina yake baada ya mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Anna kudaiwa kuwa ni mchawi na kudondokea kanisani.


Tukio hilo lililochukua saa kadhaa lilitokea katika Kanisa la Yesu Kristo la Huduma ya Maombezi na Uponyaji linaloongozwa na Nabii Flora Peter lililopo Mbezi Beach Salasala, Dar hivi karibuni.
Taarifa kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo ambao ni waumini wa kanisa hilo inadai kuwa mwanamke huyo, mkazi wa Bunju, Dar alifika kanisani hapo saa 4:45 asubuhi huku akiwa amebeba Biblia na pochi lake akionekana kuwa sawa waumini wengine.

WAUMINI WABAKI VINYWA WAZI
Ilidaiwa kuwa muda mfupi baada ya maombi kuanza, katika hali isiyo ya kawaida, mwanamke huyo aliruka kupitia dirishani akapotea na kuacha waumini vinywa wazi.
Habari zilidai kuwa kuna baadhi ya watu walimuona kwenye paa ya nyumba ya watu waliojenga karibu na kanisa hilo, hali iliyozidi kusababisha mkusanyiko mkubwa wa watu wakiwemo askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) waliokuwa wakimshangaa.
Wakati taharuki hiyo ikiendelea, mwanahabari wetu alitonywa kuwepo kwa tukio hilo ambapo aliwasha ‘tukutuku’ yake na kuwahi eneo la tukio.

NI SIMULIZI NDEFU
Akizungumzia tukio hilo, mmoja wa viongozi wa kanisa hilo aliyejitambulisha kwa jina la Octavian Mahembe alikuwa na haya ya kusema:
“Nakumbuka kulikuwa na waumini wengi kanisani, walikuja kwa ajili ya maombi, huyo mwanamke naye alikuja hapa kama waumini.
“Ilipofika saa 5:00: asubuhi watu wakawa wanasubiri maombi, baadaye nabii naye akawa amefika na kuanza kutoa maombi. Baada ya maombi kuanza, yule mwanamke alianza kuhangaika, akawa anahamahama, hatulii sehemu moja.


“Watu waliokuwa wanataka kuombewa waliambiwa wapite mbele.
“Yule mwanamke alikurupuka na kurukia ukuta wa futi sita na nusu, akadondoka nje.
“Nabii alisema afuatwe ili aombewe, alidai kwa kuwa si mtu mwema ni hatari na anaweza kuliangamiza kanisa na waumini kwa jumla kwani alikuwa na nguvu za giza.
“Alipochukuliwa akapelekwa kwa Nabii, akaombewa sala ya toba huku akikataa kwa kusema hana dhambi.
“Aliendelea kuombewa na baada ya maombi alitoka nje kupitia mlangoni. Akiwa nje alivua nguo na kubaki na ile ya ndani tu, akapanda juu ya paa la nyumba jirani na kanisa, akarukia nyumba nyingine juu kwa juu bila kushuka.
“Hakuishia hapo, akawa amerukia mti huku akionekana kama mtu wa ajabu kiasi kwamba hata watu wengine hawawezi kufanya yale aliyokuwa akiyafanya.
“Watu wengi walikusanyika wakiwemo polisi na wanajeshi. Baada ya kupotelea mitini, ghafla kilisikika kishindo kanisani baada kudondoka eneo hilo.
“Baadaye alipelekwa ofisi ya serikali ya mtaa kwa usalama wake kwani watu walitaka kuchukua sheria mikononi wakidai ni mchawi,” alimaliza kusimulia kiongozi huyo wa kanisa.




ATANGAZA ALIYOKUWA AKIFANYA
Hata hivyo, habari nyingine zilidai kwamba kabla ya mwanamke huyo kupelekwa serikali ya mtaa, wakati akiombewa alikuwa akitangaza mambo mengi aliyokuwa akiyafanya yasiyoeleweka kwa watu wasiojua mambo ya kilozi.
 
SERIKALI YA MTAA
Mwandishi wetu hakuishia hapo, alikwenda hadi ofisi za serikali za mtaa kutaka kujua kama mwanamke huyo alifikiswa hapo na sehemu alipo kwa sasa.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Salasala, Monica Timba alikiri kutokea kwa tukio hilo akidai kuwa siku hiyo hakuwepo ofisini lakini alipigiwa simu na mkazi wa eneo lake kujulishwa juu ya tukio hilo.
“Niliambiwa kuna vurugu kubwa katika mtaa wangu na kwamba kulikuwa na mchawi amedondoka kanisani,” alisema mwenyekiti huyo.
Kiongozi huyo aliendelea kusema kuwa  baada ya kupewa taarifa hiyo alimpigia simu mtendaji wake, Ramadhan Juma ili mwanamke huyo aokolewe na walifanya hivyo.



HADI KITUO CHA POLISI
Alisema kuwa baadaye mwanamke huyo alipelekwa kituo kidogo cha polisi kilichopo eneo hilo cha Mtongani.
Risasi Jumamosi lilibisha hodi kituoni hapo na kuzungumza na askari aliyekuwa zamu ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini kwa kuwa siyo msemaji wa jeshi hilo ambaye alikiri kuripotiwa kwa tukio hilo kituoni hapo.
“Ni kweli huyo mwanamke alifikishwa hapa akidaiwa ni mchawi lakini baadaye tulimwachia kwa sababu sisi hatuamini mambo ya uchawi,” alisema.    

No comments:

Post a Comment