Mbunge wa
jimbo la Igunga aliyerejeshwa na mahakama kuu Dk Peter Kafumu
akizungumza na wana Igunga mara baada ya kuwasili mjini humo leo
kuwashukuru wananchi na wapiga kura wake kwa kuwa naye bega kwa bega
katika matatizo hayo, Mkutano huo umefanyika kwenye uwanja wa Sokoine
mjini Igunga ukiongozwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri
kuu ya CCM Ndugu Nape Nnauye, amesema anaomba ushirikiano kwa kila mwana
Iguna bila kujali itikadi za vyama vya siasa.
Mbuge wa
Jimbo la Igunga Dk Peter Kafumu akihutubia mkutano wa hadhari mjini
Igunga leo kulia ni Nape Nnauye Katibu wa Itikadi na Uenezi NEC
Maelefu ya wana Igunga wakiwa katika mkutano huo leo
Wananchi wa Igunga wakipmokea mbunge wao kwa mabango yenye ujumbe wa kumkaribisha jimboni mwake
Dk Peter Kafumu akivishwa shada la maua mara baada ya kuwasili mjini Igunga
Mbunge
wa Igunda, Dk. Peter Dalally Kafumu akiwasalimia wananchi katika
mkutano wa mapokezi yake uliofanyika jioni hii kwenye Uwanja wa Sokoine
mjini Igunga mkoani Tabora. Kuliani Katibu wa NEN, Itikadi na Uenezi
CCM, Nape Nnauye.(Picha na Bashir Nkoromo)
NA BASHIR NKOROMO,IGUNGA
WAKATI mapokezi ya Mbunge wa Igunga Dk. Dalally Peter Kafumu yamesababisha baadhi ya shughuli kusimama, kwa hoi hoi, nderemo na
vifijo, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeahidi kuongeza kasi ya utekelezaji wa ahadi ilizotoa katika jimbo hilo.
Akizungumza
kwenye mkutano wa mapokezi ya Dk. Kafumu uliofanyika kwenye Uwanja wa
Sokoine mjini hapa, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye,
alisema CCM lazima itazitekeleza ahadi zote zilizotolewa na mbunge huyo
kupitia ilani ya Chama wakapi akigombea katika uchaguzi mdogo
uliofanyika 2011 jimboni humo.
“Baada
ya mahakama kumrejeshea Ubunge mbunge wetu, CCM inaahidi kwamba ahadi
zote alizotoa mbunge wenu zitatekelezwa kabla ya mwaka 2015. Na kwa kuwa
Chadema walipunguza kasi kwa kusimamisha mbunge wenu baada ya kumpeleka
mahakamani, CCM itaisimamia serikali ili kuhakikisha inaongeza kasi ya
utekelezaji wa ahadi hizo kufidia pale utekelezaji ulipokuwa umepungua
kasi”, alisema Nape.
No comments:
Post a Comment