RAIS
Jakaya Kikwete anatarajiwa kufanya kikao cha siku mbili na wabunge wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujadili masuala mbalimbali ya taifa, ikiwamo
utekelezaji wa ilani ya uchaguzi katika majimbo yao.
Katika
kikao hicho, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, anatarajiwa kuwapa
nguvu wabunge wake katika kueleza masuala mbalimbali, ikiwamo hatua ya
Serikali kupitisha bajeti, huku miradi ya maendeleo ikisuasua katika
utekelezaji kwa madai ya kukosekana kwa fedha.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Katibu wa Halmashauri Kuu,
Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema kikao hicho ni cha kazi na
kitakuwa kinatoa nafasi zaidi kwa wabunge kueleza masuala yanayoh
Nape alisema kikao hicho hakina
uhusiano wa aina yoyote na matukio yanatokea bungeni hivi sasa, bali ni
ratiba ya kikao cha kazi za Mwenyekiti katika kupima utekelezaji wa
ilani na miradi ya maendeleo katika majimbo mbalimbali ambayo yapo chini
ya wabunge wa CCM.
“Hiki ni kikao cha kazi, ninapenda
kueleweka kuwa CCM ndiyo iliyokabidhiwa jukumu la kuongoza nchi hii na
wabunge wa chama chetu ndiyo wanaisimamia ndani ya Bunge, hasa katika
kuhoji masuala mbalimbali yanayohusu nchi na watu wake.
“Lakini kutokana na hali hii, kikao
hiki kitakuwa cha siku mbili ambako siku ya kwanza itakuwa ni fursa kwa
wabunge kusema masuala mbalimbali dhidi ya serikali yao.
No comments:
Post a Comment