Watanzania
tunafuraha kubwa kwa sababu wapiganaji wa Jeshi letu la Wananchi
Tanzania (JWTZ) wamewasili mji wa Goma, Mashariki mwa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo kujiunga na mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda
amani wakiwa salama....
Wiki
iliyopita, Amiri Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete alikabidhi Bendera kwa
Kiongozi wa Bataliani ya wapiganaji wa JWTZ wanaokwenda nchini humo,
kwenye hafla iliyofanyika Msangani Kibaha, Mkoa wa Pwani.....
Siku moja
kabla ya kufika kwa kikosi cha pili cha Tanzania (cha kwanza kilienda
kimya kimya) waasi wa M23 waliendesha kampeni kubwa sana ya kuhamasisha
wananchi wa GOMA waandamane kupinga ujio wa askari wa Tanzania mjini
GOMA...
Kiongozi
wa siasa wa M23 akiongea na wakazi wa Kibumba na huku hutuba yake
ikirushwa na redio inayomilikiwa na waasi na kusikika mjini GOMA
,aliwaasa wakazi wa GOMA wafanye maandamano makubwa siku vikosi vya
TANZANIA vitakapowasili...
CHAKUCHEKESHA
ni kwamba, tofauti na waaasi walivyo tegemea , hakuna Mtu hata mmoja
aliye andamana! Hii inaonyesha wazi kuwa waasi hawa wameshapoteza
ushawishi walio kuwa nao hapo awali....
No comments:
Post a Comment