Waziri wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli.
Na Mohammed Kuyunga
WAZIRI
wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli ndiye waziri namba moja hadi sasa
kwa kulivunja mbavu Bunge la Bajeti linaloendelea mjini Dodoma kutokana
na vichekesho vyake wakati alipokuwa akijibu hoja za wabunge mbalimbali
hivi karibuni.
Magufuli
ambaye wengi humuita ‘Jembe’ kutokana na uchapa kazi wake, alikuwa
akiwasilisha bajeti ya wizara yake na kuomba kuidhinishiwa Shilingi
Trilioni 1.22 kwa mwaka wa fedha 2013/14.
Mheshimiwa
huyo alimudu kuwafanya waheshimiwa wacheke sana huku ujumbe ukifika
tofauti na mawaziri wengine waliopita ambao hotuba zao zinadaiwa kuwa
zilijaa ushawishi wa usingizi.
“Tunajenga
barabara kwa kiwango cha lami kutoka Dodoma kwenda Iringa, wale watani
zangu wa Iringa hawatakuwa na haja ya kujinyonga kwenye miti, sasa
watakuwa wakilala barabarani tu.”
Wabunge
walivunjika mbavu kwa vicheko. Watani zake alimaanisha Wahehe ambao
inadaiwa wanapokuwa na hasira wana tabia ya kujiua kwa kujinyonga (ni
madai).
Kama
vile haitoshi, waziri huyo akijibu swali la Mbunge wa Same Mashariki,
Mheshimiwa Anne Kilango Malecela kuhusu barabara inayopita kwenye
Kiwanda cha Tangawizi kupewa hadhi, pia alitumbukiza utani.
“Mheshimiwa
Anne Kilango yale uliyosema tunayafanyia kazi, kuhusu barabara
inayopita Kiwanda cha Tangawizi kupewa hadhi tumepokea, maana pia
mheshimiwa rais alitupa maagizo.
“Nimeamini
una akili sana ndiyo maana mtani wangu Malecela alitoka Dodoma na
kwenda milimani Same huko, kwa nini hakuja usukumani?”
Aidha,
waziri huyo akimjibu Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari ambaye
alitoa ushauri kwa Wizara ya Ujenzi kupunguza idadi ya miradi na
kukamilisha mmoja baada ya mwingine ili wizara iweze kufanikiwa huku
akilalamikia kutojengewa barabara jimboni kwake, Magufuli aliwavunja
mbavu tena wabunge:
“…ushauri
wako ni mzuri ndiyo maana wizara yangu imeamua kuacha kujenga barabara
jimboni kwako ili tukamilishe sehemu nyingine kwanza…”
Hata
hivyo, wakati wabunge wakivunjika mbavu, Magufuli alisema Serikali ya
Chama Cha Mapinduzi (CCM) haina ubaguzi na itajenga barabara hiyo
iliyoko jimboni kwa mbunge huyo.
Akimjibu
Mbunge wa Viti Maalum (CCM –Bunda), Ester Bulaya ambaye alisema kwamba
anamkubali waziri huyo kutokana na utendaji wake, Magufuli naye
alisimama na kusema:
“Hata mimi namkubali Ester Bulaya...”
Aidha,
Magufuli aliwashangaa wabunge wa upinzani ambao walionesha kutaka
kumpinga na kuwaambia kuwa bosi wao, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman
Mbowe alionesha kumkubali na kuzimwagia sifa sera za CCM baada ya
kukamilishiwa barabara iliyoko jimboni kwake Hai, Kilimanjaro.
“Kama
kuna mtu anabisha ushahidi uko hapa aje nimuoneshe, mheshimiwa
aliandika kwenye mtandao (akautaja jina zima) kisha akasema kama mtu
haamini akatoa flashi yenye sauti aliyodai ni ya Mbowe.
VIDOKEZO VINGINE:
Alimwambia mbunge wa upinzani ana moyo wa CCM CCM, amekaa ki-CCMCCM.
Katika kutekeleza uvunjaji wa nyumba zilizoingilia hifadhi ya barabara aliwahi kuvunja ukuta wa nyumba ya baba yake mzazi.
No comments:
Post a Comment