Pages

Thursday, May 2, 2013

WABUNGE WATWANGANA NGUMI NDANI YA BUNGE.




Bunge la Venezuela.
Makonde yameibuka bungeni na baadhi ya wabunge kujeruhiwa katika sintofahamu, kutokana na mjadala kuhusu uchaguzi wa hivi karibuni unaobishaniwa.

Upande wa upinzani ulisema juzi kwamba wabunge wao saba, walishambuliwa na kujeruhiwa wakati wakipinga hatua ya kuwazuia kuzungumza katika Bunge hilo, kutokana na kukataa kwao kutambua ushindi wa Rais Nicolas Maduro uliofanyika Aprili 14. 
Wabunge wa chama tawala walilaumu wapinzani wao hao na kuwaita mafashisti kwa kuanzisha vurugu, hali iliyoonesha siasa tete katika Taifa hili mwanachama wa OPEC baada ya kifo cha Msoshalisti, Hugo Chavez mwezi jana.

  
“Tulijua wapinzani wamekuja hapa kuanzisha ghasia,” Maduro alisema kutokana na tukio hilo. “Hii haipaswi kujirudia.” Maduro (50), ambaye aliteuliwa na Chavez kuwa mrithi wake, alimshinda mgombea wa upinzani Henrique Capriles kwa asilimia 1.5 za alama. Capriles (40) amekataa kutambua ushindi wake, akidai kuwapo kwa idadi kubwa ya upungufu na kwamba kura ziliibwa. Uchaguzi huo ulibainisha mgawanyiko dhahiri wa Taifa hili baada ya miaka 14 ya utawala wa kisoshalisti wa Chavez. 

No comments:

Post a Comment