Mkurugenzi mkuu wa Montage Limited Company, Ms Teddy Mapunda akiteta jambo na Joyce Mhavile Mkurugenzi wa ITV
katika hafla hiyo ya kutoa msaada wa shilingi milioni 70 kwa WAMA ikiwa
ni kuchangia juhudi za serikali, mashirika na wadau kupambana na tatizo
la vifo vya mama wajawazito na watoto nchini Tanzania
Mke
wa rais wa Jamhuri wa Tanzania na mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma
Kikwete akipeana mkono wa furaha na Joyce Mhavile baada ya kupokea
msaada huo muhimu kwa ajili ya kujali afya ya mama na mtoto hasa kulenga
kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto, kulia ni Mkurugenzi wa
Montage Limited Teddy Mapunda.
Ni
muhimu sana kwa makampuni mbalimbali kujali suala hili ili kutokomeza
kabisa tatizo hili katika jamii ya kitanzania. Montage Limited Company
wameonesha mfano mzuri kwa wadau wengine na lazima moyo wa utu kama huu
uigwe na wengine.
Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na menyekiti wa WAMA, Mama
Salma Kikwete akizungumza katika hafla hiyo baada ya kupokea msaada wa
shilingi milioni 70.
Mama Salma amelishukuru sana kampuni ya Montage Limited kwa msaada huo na kuyataka makampuni mengine kuiga mfani huo mzuri
Mke
wa rais na mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akipokea mfano wa
hundi ya shilingi milioni 70 kutoka ka mkurugenzi wa Montage Limited
Company, Ms Teddy Mapunda. Zoezi hilo la kuigwa limefanyika wikiendi hii
jijini Dar es salaam ili kuchangia juhudi za kujali afya ya mama
wajawazito na watoto. (Katikati) ni Mkurugenzi wa ITV, Joyce Mhaville,
(Wapili kushoto) ni Montage Director of Finance, Ms Zainabu Mkindi,
(Kulia) ni Mwanahamisi Kitogo na katibu wa foundation Mr Daud Nassib
Mke
wa rais na mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akipokea mfano wa
hundi ya shilingi milioni 70 kutoka ka mkurugenzi wa Montage Limited
Company, Ms Teddy Mapunda. Zoezi hilo la kuigwa limefanyika wikiendi hii
jijini Dar es salaam ili kuchangia juhudi za kujali afya ya mama
wajawazito na watoto. (Katikati) ni Mkurugenzi wa ITV, Joyce Mhaville,
(wa pili kutoka kushoto) ni Montage Director of Finance, Ms Zainabu
Mkindi, (Kushoto) ni Mwanahamisi Kitogo na (kulia) ni katibu wa
foundation Mr Daud Nassib
No comments:
Post a Comment