Viongozi wa serikali ya Tanzania na Marekani, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Shamsi Vuai Nahodha (kushoto) na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Alfonso Lenhardt (kulia) wakionyesha nyaraka mbili za Mpango wa kukabiliana na maradhi ya mafua ya ndege. Nyaraka hizo zinahusisha vikosi vya jeshi na raia nchini Tanzania na Kamandi ya Jeshi la Marekani la Kupambana na Majanga Barani Afrika (USAFRICOM).Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Shamsi Vuai Nahodha akizungumza na viongozi mbalimbali wa vitengo vya kukabiliana na majanga kutoka Tanzania na Marekani leo jijini Dar es salaam.Pamoja na mambo mengine amesema Tanzania inaendelea kujenga uwezo wa ndani wa kukabiliana na majanga mbalimbali.
Balozi wa Marekani nchini Tanzania Alfonso Lenhardt akiongea na viongozi mbalimbali wa vitengo vya kukabiliana na majanga kutoka Tanzania na Marekani leo jijini Dar es salaam na kusisitiza kuwa serikali ya Marekani itaendelea kushirikiana na Tanzania na nchi nyingine katika kukabiliana na majanga yanayotokea.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wa siku mbili kutoka Tanzania wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Shamsi Vuai Nahodha akitoa ufafanuzi kwa waandishi kuhusu utayari wa Tanzania katika kukabiliana na majanga mbalimbali yanayotokea kwa kuvishirikisha vikosi vya ulinzi na usalama, wataalam wa sekta nyingine, utoaji wa tahadhari mapema kwa wananchi na uimarishaji wa kitengo cha maafa nchini.
No comments:
Post a Comment