Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, June 29, 2013

Balozi Sefue naye aungana na Pinda


WAZIRI MKUU PINDA NA KATIBU MKUU KIONGOZI, BALOZI SEFUE

KATIBU Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, ameunga mkono kauli iliyotolewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ya kutoa kibali kwa Jeshi la Polisi kuwapiga watu wanaokaidi amri halali. Akizungumza Dar es Salaam jana, alisema kauli hiyo imewatoa wasiwasi Watanzania wapenda amani, huku ikiongeza hofu kubwa kwa wahalifu wenye nia mbaya na Serikali.

Alisema baada ya Pinda kutoa kauli hiyo, Watanzania walio wengi walifarijika huku waliokuwa na malengo ya kuivuruga Serikali kulalamika kwa kutoa sababu zisizojenga umoja na mshikamano tulionao.

“Kwanza kauli hii imemfurahisha Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Said Mwema kiasi cha kumuongezea kasi ya kusimamia zaidi usalama wa raia na mali zake.

“Sikubaliani kamwe na tuhuma zinazoelekezwa kwa Pinda na baadhi ya wachache waliokuwa na mbinu chafu, tathimini inaonyesha Watanzania wamefarijika na kuondolewa na wasiwasi.

“Nawaomba raia wote waishi kwa imani na Serikali imejiimarisha sehemu zote kuhakikisha nchi inabaki na sifa yake kuwa ni kitovu cha amani duniani,” alisema Balozi Sefue.

No comments:

Post a Comment