Pages

Monday, June 24, 2013

HATIMAYE JESHI LA POLIS WAMJIBU JOYCE KIRIA KUHUSU MADAI YAKE KWAMBA WAMWAMBIE ALIPO MUME WAK

Advera-SensoInasikitisha kuona kwamba huyu mama Joyce Kiria anaingilia mambo ya kisheria na kutaka kupotosha jamii kwamba hajui mume wake yuko wapi pia nadhani analenga kuichochea jamii kwamba aliyetuhumiwa kutenda uhalifu akikamatwa familia yake iandamane, tendo ambalo pia ni kosa la jinai. Aidha anatakiwa kuheshimu haki za watoto na kuacha kuwatumia katika kinga ya kutetea watu wanaotenda uhalifu (Imetolewa na Advera Senso Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini Tanzania)
1aJoyce Kiria akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam ambapo alidai hajui mume wake yuko wapi

NAOMBA MSAADA KWA RAISI WANGU WA NCHI, IGP SAID MWEMA, WANAWAKE WENZANGU NA WATANZANIA WOTE KWA UJUMLA". KUJUA MUME WANGU ALIPO.JOYCE KIRIA




Baada ya kukaa kwa siku mbili bila kujua alipo mume wangu, nimejitokeza mbele ya waandishi wa habari wapate kunisaidia kufikisha ujumbe wangu wa kupata msaada ya kujua mume wangu alipo.

Hapa ni karibu kabisa ya ukumbi wa habari maelezo ambapo niliwafuata waandishi wa habari ili kupata muda wa kuongea nao, nikiwa nimewabeba wanangu Lincon na Linston.

Nina watoto wawili mkubwa ni wa miaka 2 na mdogo wake ni wa miezi 4, leo ni siku ya nne hawajamuona baba yao, baba yao ni msaada mkubwa mno kwa familia yangu, Raisi Kikwete huko ulipo nakuomba usikie kilio changu, IGP Said Mwema nahitaji msaada wako, Wanawake na Wote nahitaji msaada wenu.


Hapa nikiendelea kuelezea hali halisi ya jambo hili mpaka leo hii kuja hapa, na kubwa ni kutopewa taarifa ya mume wangu alipo. Sina Amani kabisa naomba kupata taarifa kamili huko aliko yuko salama? na hata kufahamu anakula nini?

Kubwa watanzania wenzangu ni kunisaidia katika maombi ili huko aliko awe salama.

Kwa Urefu zaid habari hii itaruka katika vyombo mbalimbali vya habari zikiwepo TV kama Channel Ten, ITV, EATV, Star TV na Clouds, Radio kama Clouds, Radio One, na magazeti kama Mwananchi, Nipashe , Mtanzania, Tanzania Daima , The Citizen, Guardian, na vyombo vingine vya habari.

Nawashukuru waandishi wote ambao walikuwepo hapa, pia na watanzania wote naamini mko pamoja na mimi. .
 

No comments:

Post a Comment