Pages

Thursday, June 27, 2013

HATUA KALI NA ZA HARAKA ZINAHITAJIKA KUOKOA MAISHA YA HUYU BINTI AMBAYE AMENUSURIKA KUNYONGWA NA MUME WAKE AMBAYE NI POLISI HUKO IRINGA.


Hapa Rehema akiwa wodini katika Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa alipokimbizwa kwa matibabu kutokana na kipigo kikali toka kwa askari huyo, ambaye ni mume wake.Haya ni baadhi ya majeraha ambayo aliyapata shingoni kutokana na kukabwa shingo na askari huyo.

Bi Rehema akiwa nyumbani kwa wazazi wake baada ya kukimbia nyumba yake kutokana na kipigo kisichokwisha 
Mama mzazi wa Rehema akiwa Monica Shauri
 
Rehema Shauri Madongo ni mmoja kati ya mwanamke ambaye amebahatika kuolewa na askari polisi kitendo cha upelelezi ambaye anaeleza jinsi alivyotendewa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kuteswa na kupigwa kikatili na pindi anapofika polisi hakuna hatua zozote zinazochukuliwa kwa mtuhumiwa huyo ambaye ni askari .

 Kwa alisema toka ameolewa kila mara amekuwa akipokea kipigo na mbaya zaidi kabla ya kupigwa amekuwa akifungwa mikono kwa pingu zinazotumika kuwafunga watuhumiwa pingu ambazo mume wake huyo amekuwa akizihifadhi ndani ya nyumba. 
" Kweli inasikitisha sana kusimulia kwani kabla ya kupigwa nimekuwa nikifungwa pingu mikono kama mharifu sugu na baada ya hapo kipigo kikali kimekuwa kikinikuta ....hadi sasa nimepigwa zaidi ya mara 20 na polisi nimekwenda kuripoti mara tatu na Hospital nimelazwa mara moja ila siku nyingine nimekuwa nikiugulia nyumbani ila nyumbani kwa wazazi nimerudi mara tatu sasa"
Alisema kuwa mbali ya kupigwa na kuumizwa ila kuna mateso mengine ambayo amekuwa akiyapata kutoka kwa mwanaume huyo ni siri yake na hayapaswi kuelezwa hapa kutokana na jinsi ambavyo askari huyo anavyomtenda ukatili wa kinyama. Hata hivyo alisema kuwa akiwa na mimba ya mwezi mmoja hali ya kipigo ilizidi zaidi na wakati mwingine alipata kumfunga shingo na kanga kwa kutaka kunyonga shingo huku akitishi kumuua
Aidha alisema kuwa kila akifika polisi kufungua kesi hakuna utekelezaji unaofanyika kutokana na polisi kulindana  kwa suala hilo. Pia alisema mbali ya kupigwa akiwa nyumbani kwake ila bado anapoamua kukimbia nyumba hiyo na kukimbilia kwa wazazi wake bado askari huyo amekuwa akimfuata na kumpa kipigo mbele ya wazazi wake, tendo ambalo limempelekea yeye na Mama yake
wamekuwa wakiishi ndani wamejifungia milango kuogopa askari huyo kuja kuwafanyia ukatili, ikiwa ni pamoja na kuwaua kwa risasi kama ambavyo amekuwa akiwatisha mara kwa mara.
Bi Shauri alisema mbali ya kuwa yeye ni mmoja wa wacha Mungu kwa maana na Mlokole mzuri ambae kila wakati asubuhi lazima aende kusali ila kwa sasa anaogopa kutoka asubuhi kwa kuhofia kuvamiwa na askari huyo . Hivyo aliomba jeshi la polisi kuweza kumpa ulinzi yeye na familia yake ama kumkamata mtuhumiwa huyo ambae inadaiwa kwa sasa yupo katika mji wa Iringa. 

No comments:

Post a Comment