Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, June 30, 2013

KATIBU WA CHADEMA WILAYA YA MAKETE ATUPWA JELA MIEZI 9 KWA KOSA LA KUTOTII AMRI YA POLISI

 


Mahakama ya mwanzo Makete mjini wilayani Makete mkoani Njombe imemuhukumu katibu wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wilaya hiyo Bw Godfrey Mahenge (63) kwenda jela miezi 9 kwa kosa la kutotii amri halali ya jeshi la polisi Makete

Akitoa hukumu hiyo hakimu wa mahakama ya mwanzo Makete mjini Mh. John Mpitanjia amesema mtuhumiwa huyo alitumia lugha ya matusi kwa askari polisi na kuwaita kuwa ni wauaji na kudai kuwa wametumwa na chama cha mapinduzi (CCM)



Amesema baada ya mahakama yake kuridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashataka, mshtakiwa alitakiwa kutumikia kifungo cha miaka miwili gerezani lakini kutokana na kutenda kosa hilo kwa mara ya kwanza mahakama imeamua kumfunga miezi 9 gerezani ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo..



Mshtakiwa huyo hakuwa na lolote la kijitetea na hakimu kumpatia adhabu hiyo na kusema kuwa rufaa kwa mshtakiwa ipo wazi endapo anahisi ameonewa.

No comments:

Post a Comment