Waumini
wa dini ya Kiisilamu wakiwa kwenye Kongamano lililofanyika leo jijini
Dar es Saalaam kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo mada mbalimbali
ziliwasilishwa na masheikh. Msimamo wa waisilamu juu ya Maendeleo ya
mchakato wa katiba mpya, Dhulma na uonevu dhidi ya waisilamu pamoja na
hatua za kuchukuwa kama madai yao yatapuuzwa.
|
Hivi ndivyo Diamod ilivyofurika. |
|
Waisilamu wa Rika na jinsi zote walikuwepo. |
|
Imamu wa Msikiti wa Mtambani Imam Suleiman akimkaribisha Sheikh Ponda kuhutubia waisilamu kwenye Kongamano hilo. |
|
Takibirrrrr zikafuatia baada ya kukaribishwa Sheikh Ponda. |
|
Sheikh Konda Juma Bungo nae aliwasilisha mada. |
|
Sheikh Ponda Issa Ponda (kushoto) akihutubia waisilamu kwenye kongamano hilo. |
|
Sheikh
Ally Basaleh nae hakusita kuwaambia serikali kuwa kwenye daladala
waliopanda watanzania kuna watu wamevaa ndala na kuna wengine wamevaa
buti wenye ndala wanakanyagwa ndio maana wanasema! Kwahiyo badala ya
kufanya hasira na kuchukua maamuzi ya nguvu bora wawasikilize wanaosema wanakanyagwa. |
|
Amiri
wa Jumuia na Taasisi za Kiisilamu Tanzania Sheikh Musa Kundecha nae
aliwaambia waisilamu kuwa kwa kawaida mtu akilala ukimwamsha huamka
lakini ukimwona amelala una mwamsha na haamki basi ujue hajalala ila
anajifanya amelala dawayake ni kumkera mpaka aamke.
|
|
Jopo la Masheikh wa Meza kuu |
Na Mwandishi Maalum.
WAISILAM leo
wametoa msimamo juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea nchini wakati
wa kongamano lililoandaliwa na jumuiya na Taasisi za Kiisilamu Tanzania
jijini Dar es Salaam.
Kwenye
kongamano hilo ambalo masheikh mbalimbali wakiwemo Sheikh Ponda Issa
Ponda, Ally Basaleh, Mussa Kundecha na Kondo Juma Bungo waliwasilisha
mada mbalimbali pamoja na kutangaza maazimio ya kongamano hilo.
Moja
ya mambo yaliyozungumzwa ni mapendekezo waliyowasilisha kwenye Tume ya
katiba mpya ambapo walisema iwapo mapendekezo waliyowasilishwa
hayakuzingatiwa na kutupwa yote basi waisilamu watatangaza kusimamisha
mchakato huo nchi nzima na kufanya maandamano usiku na mchana.
Hoja
hiyo ilikuja baada ya kunukuliwa kauli ya Waziri wa nchi Sera na
Uratibu wa bunge Wiliam Lukuvi, wakati akijibu swali la Mbunge Asumta
Mshama aliyetaka kujua kwamba lini serikali itaacha kupanga siku ya
kupiga kura kuwa Jumapili wakati wanajua siku hiyo ni siku ya ibada ya
wakristo haioni inawadhulumu hakiyao yakufanya ibada?, Lukuvi kwenye
jibu lake alisema suala hilo limekuwa likilalamikiwa na watu wengi tu
lakini serikali kwenye hilo haina utaratibu maalum wa siku ya kupiga
kura ila kwakuwa kuna mchakato wa katiba mpya hilo litazingatiwa.
“Hii
ni kinyume kabisa na utaratibu wa tume ya katiba waziri huyu anataka
tuamini kwamba anayafahamu yatakayokuwemo kwenye katiba mpya kabra hata
wananchi hawajapelekewa na hata haijaandikwa? Hivyo iweje waisilamu
wanaodai siku ya ijumaa iwe ya mapimziko kwa miaka nenda rudi hawapewi
wakristo wanakosa sikumoja tu ndani ya miaka mitano majibu yanapatikana
kirahisi?” Alihoji sheikh Ponda.
“W
aisilamu wamekuwa wakiomba ruhusa kwa mabosi wao siku ya ijumaa kwenda
kufanya ibada na mara nyingine wananyimwa ruhusa hiyo lakini hakuna
vurugu yeyote waliofanya na wanadai haki hiyo kwa miaka yote hii lakini
hawapewi lakini wengine wanadai kirahisi na kujibiwa kwa uhakika.”
Alifafanua.
Aidha
heikh Ponda alifafanua kuwa waisilamu wavumilie wasubiri rasimu
itakapotangazwa kwenye magazeti ya serikali kama mapendekezo
waliyowasilishwa yatapuuzwa basi hakuna katiba mpya maandamano usiku na
mchana mpaka kieleweke nchi nzima.
Sheikh Ally Basaleh alisihi Serikali kuwasikiliza waisilamu hoja zao wasiwapuuze.
|
No comments:
Post a Comment