Pages

Saturday, June 29, 2013

LIGI KUU YA NETIBOLI TAIFA KUFANYIKA JIJINI MBEYA KWA MARA NYINGINE!!


 

IMG_4505
Kwa mara ya pili mfululizo, jiji la Mbeya litakuwa mwenyeji wa ligi kuu ya Netiboli taifa ambapo  naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo anatarijiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi kuanzia Agosti 24 hadi Septemba 7.
Mwenyekiti wa chama cha Netiboli Mkoa wa Mbeya, Mary Mung’ong’o ameumabia mtandao huu kuwa ligi hiyo inafanyika kwa mara nyingine kutokana na ombi la Waziri Mulugo kwa vile ligi hiyo haikuwa imefana, hivyo akaiomba CHANETA kuwapa Mbeya fursa nyingine ya uwenyeji.
Alisema maandalizi ya ligi yameanza na kusema zinahitajika sh milioni 16 kufanikisha na kuongeza kuwa hadi sasa, hawajajua timu ngapi zitashiriki kutokana na jukumu hilo kuwa chini ya Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA).
Hata hivyo, mwenyekiti huyo alitoa wito kwa viongozi wa ngazi mbalimbli wakiwemo wadau wenye mapenzi na mchezo kutoka mkoani hapa kujitoa kwa hali na mali kuyafanikisha ili yawe chachu ya kukua kwa mchezo huo nchini kwa maslahi ya vijana na taifa.
Aidha, mwenyekiti huyo alitamtambulisha Nwaka Mwakisu kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano hayo.
Akizungumzia mashindano hayo, Mwakisu alisema ni fursa kwa watu wa Mbeya kujitangaza kibiashara kupitia mchezo huo na kufuta makosa yaliyofanyika mwaka jana.
Alisema katika kufakisha mashindano hayo, nguvu ya pamoja inahitajika kuanzia viongozi wa kisiasa, serikari na vyombo vya habari.

No comments:

Post a Comment