Wananchi
wa Zizi la Ng'ombe mjini Iringa wakiwa kando ya gari ambalo marehemu
alijificha chini ya uvungu baada ya kupigwa risasi na majambazi hao
Mwili wa marehemu huyo aliyetambulika kwa jina la baba Daudi ukiwa katika gari la polisi
Huu ndio mwili wa marehemu huyo baada ya kupigwa risasi na watu wanaosadikika kuwa ni majambazi leo
Askari polisi wakiushusha mwili huo tayari kuuhifadhi chumba cha maiti Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa
Jeraha ambalo kijana Patrick Vatung'a alilojeruhiwa kwa risasi
Majeruhi wa risasi Dismas Nyaulingo kulia na Patrick Vatung'a wakiwa wodini jana
WAKATI
kikao cha wadau wa ulinzi kinataraji kufanyika leo jumanne mkoani
Iringa katika ukumbi wa Siasa ni kilimo kikao kinacholenga kupambana
na mtandao wa uharifu mkoa ya kusini mwa Tanzania ,
Watu
wanaosadikika kuwa ni majambazi wakiwa na silaha wamevamia maduka
eneo la Zizi la Ng'ombe jirani na msikini mjini Iringa na kuua mtu mmoja
na kujeruhi wengine wawili kwa risasi kabla ya kupora fedha kiasi
cha zaidi ya shilingi milioni 2 .
Mashuhuda
wa tukio hilo wameueleza mtandao huu baada
ya kufika eneo la tukio kuwa majambazi hao wakiwa zaidi ya wawili
walivamia eneo hilo muda wa saa 1.30 usiku wa leo .
Mashuhuda
hao walisema kuwa majambazi hao baada ya kufika katika eneo hilo la
kibanda cha M-Pesa kinachomilikiwa na Zamoyoni na kufanikiwa
kumpora kiasi hicho cha fedha kabla ya kuelekea katika duka moja
wapo maarufu eneo hilo kwa lengo la kuvamia na kupora.
Alisema
Kevin Kalinga kuwa chanzo cha kuuwawa kwa mwananchi huyo
aliyetambuliwa kwa jina la baba Daudi ni kutokana na kugoma kutii amri
ya majambazi hao ambao walimkuta akitoka dukani kununu sigara na
kumtaka kukaa chini na baada ya marehemu huyo kugoma kukaa chini ndipo
walipomfyatulia risasi mwili jirani na pega na kupelekea kutimua
mbio na kujificha chini ya gari lililokuwa limeegeshwa nje ya duka
hilo gari aina ya Toyota Hilux lenye namba T 258 .
Hata hivyo
baada ya kupigwa risasi kwa mwananchi huyo wananchi waliokuwa
karibu na eneo hilo walianza kujikusanya kwa lengo la kuwavaa
majambazi hao hali iliyopelekea majambazi hao kuanza kufyatua
risasi ovyo na kujeruhi wananchi waliokuwa karibu na eneo hilo.
Kwa upande
wao majeruhi wa tukio hilo ambao wamelazwa wodi namba 5 katika
Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa Dismas Nyaulingo ( 20) na Patrick
Vatung'a(19) walisema kuwa wao walikuwa wakiendelea kucheza Pool
eneo hilo na baada ya kusikia mlio kama wa baruti walianza kujihami
kwa kukimbia na ndipo walipokutwa na mkasa huo .
Nyaulingo
alisema chanzo cha majambazi hao kuanza kufyatua risasi onyo ovyo ni
baada ya wananchi kuanza kujikusanya kwa lengo la kupambana na
majambazi hao .
"Sisi
tulikuwa tukicheza mchezo wa Pool eneo hilo na baada ya hapo tulisikia
mlio wa risasi hewani na tukajua ni baruti na baada ya kusikia mlio
wa pili ndipo tulipoanza kutimua mbio kabla ya kupigwa risasi "
Nyaulingo
yeye amedai kujeruhiwa eneo la paja lake la mguu wa kushoto huku
mwenzake Vatung'a akijeruhiwa eneo la paja la mguu wa kulia.
Madaktari waliowatibu majeruhi hao wamedai kuwa hali zao zinaendelea vizuri na uwezekano wa kupona ni mkubwa zaidi.
Tukio hili
limetokea ikiwa ni siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete
kumpandisha cheo aliyekuwa kamanda wa polisi mkoa wa Iringa (RPC)
Michael Kamuhanda ambae kutokana na kupanda kwake kwa cheo wakati
wowote kuanzia wiki hii atauaga rasmi mkoa wa Iringa na kwenda kuanza
maisha mapya katika kiti cha enzi mpya.
source www.francisgodwin.blogspot.com
No comments:
Post a Comment