Pages

Thursday, June 27, 2013

Mbaspo yatoa onyo Airtel Rising Stars - Yailarua Mbeya Sekondari 6-0

 Beki wa timu ya Faru Boys Nassoro Dibagula (kushoto) akitoa  mpira katika eneo la hatari  mbele ya  Abdalah Juma wa Mapambano katika mechi ya ufunguzi wa michuanoa ya  vijana wenye umri  chini ya miaka17  ya Airtel Rising Star,. Mkoa wa Temeke, uliofanyika kwenye uwanja wa Twalipo jijini Dar es Salaam Juni 25, 2013. Faru Boys ilishinda 1-0.
 Beki wa mapambano  Hamisi Hassan akimvuta jezi beki wa Faru Boys Nassoro Dibagula  katika mechi ya ufunguzi wa michuanoa ya  vijana wenye umri  chini ya miaka17  ya Airtel Rising Star,. Mkoa wa Temeke, uliofanyika kwenye uwanja wa Twalipo jijini Dar es Salaam Juni 25, 2013. Faru Boys ilishinda 1-0.
Afisa uhusiano na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki, akikagua timu wakati wa uzinduzi wa michuano ya Airtel Rising Stars katika mkoa wa kisoka wa Temeke ambapo Faru Boys football ilichuana na timu ya Mapambano katika mechi ya ufunguzi
Timu ya Mbaspo Academy ilifanya mauaji juzi Jumanne kwa kubamiza bila huruma timu ya Mbeya Sekondari 6-0 katika mashindano yanayoendelea ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars ngazi ya mkoa. Mechi hiyo ilichezwa kwenye kiwanja cha Magereza mkoani Mbeya.
Washindi walifungua kitabu chao cha magoli katika dakika ya sita kupitia kwa mshambuliaji wao mahili Jackson Mwaibale aliyefunga magoli manne peke yake. Mshambuliaji huyo kinda aliifungikia tena timu yake magoli matatu katika dakika za 16, 20 na 74. Wanafunzi wa shule ya sekondari Mbeya waliokuja kushangilia timu yao walijikuta kwenye hali ya kukata tamaa baada ya  timu yao kuwanyong’onyesha na wapinzani wao Mbaspo. 
Peter Noah, mshambuliaji mwingine hatari wa timu ya  Mbaspo, aliifungia tena timu yake katika dakika ya 30. Alikua ni yeye tena katika dakika ya 68 alipoitimisha kalamu ya magoli baada ya kuwapita walinzi wa Mbeya Sekondari na kumuacha golikipa akiduwaa baada mpira kutinga wavuni.
Kwa upande mwingine timu ya Faru Boys football walipata ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya wapinzania wao Mapambano katika mechi ya ufunguzi ya ARS, katika mkoa wa Temeke uliofanyika katika uwanja wa Twalipo jumanne jioni jijini Dar es Salaam.
Timu zote zilianza mchezo kwa kasi na babada ya kosa kosa za hapa na pale hatimaye Yohana Joseph ilifanikiwa kuitoa kimasomaso timu yake alipounganisha krosi kutoka upande wa kushoto ambayo iliingia moja kwa moja wavuni. Goli hili lilipokelewa kwa furaha na washabiki wa Faru.
Mchezo mwingine wa Another Airtel Rising Stars, mkoa wa Ilala, ilichezwa kwenye kiwanja cha soka cha shule ya sekondari ya Benjamin William Mkapa ambapo timu ya Amana Shooting ilishinda 2-0 dhidi ya Msimamo Youth Academy. Magoli hayo yalipatikana kupitia kwa Isiaka Mohamed dakika ya  22 na Ally Shaban dakika ya 68.
Mkoa wa Mwanza ulitarajia kuzindua mechi zake za ARS ngazi ya mkoa leo, Juni 26 wakati  Morogoro na Mbeya walitarajiwa kuendeleza na mechi za mashindano hayo leo, Juni 26, 2013.
Wakati huo huo, mkoa wa kisoka wa Kinondoni umetangaza kombaini yao ya wachezaji 15 watakaowakilisha mkoa huo kwenye mashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa yatakayofanyika wenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 2  hadi 7.
Wachezaji hao ni Hamza Mohamed, Hamza Abdallah, Twalib Athuman, Fred Bakari, Hazzad Jumanne, Salim James, Abubakary Mohamed, Willy Kalolo, Didas Proches, Mustafa Yusuf, Rashid Khalifan, James Msuva, Isiaka Lukana, Ally Amin na Shabani Idd.

No comments:

Post a Comment