Pages

Wednesday, June 5, 2013

MKAZI WA LUDEWA AFARIKI KWA KUFUKIWA NA KIFUSI MACHIMBONI NJOMBE.



Kulia ni Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Focus Malengo athibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Na Prosper Mfugale Njombe.
Mkazi Mmoja wa Wilayani Ludewa Mkoani Njombe Kosmas Luoga Amefariki Dunia Baada ya Kufukiwa na Kifusi Wakati Akichimba Madini ya Dhahabu Katika Mgodi wa Kienyeji Ulioopo Wilayani Humo.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Focus Malengo AmethibitishaKutokea Kwa 
Tukio Hilo na Kusema Kuwa,Tukio Hilo Limetokea June 3  Mwaka Huu Majira ya Jioni Katika Kitongoji Cha Aman Tarafa  ya Lugarawa.
Amesema Marehemu Alifukiwa na Kifusi Wakati Akiendelea na Shughuli Zake za Uchimbaji wa Madini na Hivyo Jeshi la Polisi Linaendelea na Uchunguzi wa Tukio Hilo Huku 

Likiwashauri Wananchi Kuwa Makini Ili Kupunguza Matukio ya Aina Kama Hiyo.
Wakati Huo Huo Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Linawashikilia Watu 37 Kwa Tuhuma Mbalimbali na Ambao Wanatarajiwa Kufikishwa Mahakamani Wakati Wowote.


No comments:

Post a Comment