Meneja
wa bia ya Serengeti Allan Chonjo (wa pili kulia) akiongea kwa njia ya
simu na mshindi wa droo ya pili ya Winda na Ushinde Mwl.Michael
Valerian Mbuya katika mkutano na wana habari uliofanyika jana katika
ofisi za Kampuni ya Bia ya Serengeti jijini Dar es Salaam, kushoto kwake
ni Meneja mauzo wa Push Mobile Rugambo Rodney,
kulia kwake ni Afisa mwandamizi kutoka PWC Daniel Nnko na Mkaguzi
kutoka Bodi ya Michezo ya Bahati Humudi Abdul Hussen(wa kwanza kushoto). Meneja
wa bia ya Serengeti Allan Chonjo(katikati) akiongea na wana habari
wakati wa kumtangaza mshindi wa droo ya pili ya Winda na Ushindekatika
mkutano uliofanyikajana katika ofisi za Kampuni ya Bia ya Serengeti
jijini Dar es Salaam. Wakihakiki
namba za simu za mshindi wa droo ya pili ya Winda na Ushinde
iliofanyika jana katika ofisi za Kampuni ya Bia ya Serengeti, wa kwanza
kulia ni Meneja wa bia ya Serengeti Allan Chonjo,
Afisa mwandamizi kutoka PWC Daniel Nnko(katikati) na Mkaguzi kutoka
Bodi ya Michezo ya Bahati Nasibu Humudi Abdul Hussen(kushoto)
………………………………………………………………………
Mshindi asherekea kitita cha 1,000,000 huku akiwapongeza kampuni ya bia ya Serengeti kwa promosheni hiyo.
Kampuni
ya bia ya Serengeti imetangaza mshindi wa pili wa kampeni ya Winda na
Ushinde ambae amejinyakulia kitita cha milioni moja baada ya kuchezesha
droo yake ya pili. Droo hiyo ilichezeshwa katika ofisi za kiwanda hicho
jijini Dar es Salaam huku ikishuhudiwa na mhakiki kutoka katika bodi ya
uchezeshaji promosheni bwana Humud Abdul Hussein.
Baada
ya kupokea Michael Varelian Mbuya (29) ambae ni mwalimu wa sekondari
kutoka Tabata Dar es salaam alionesha furaha yake na kubaki bumbuwazi
kwa furaha. “Nina furaha isiyokifani kuwa mshindi wa promosheni hii ya
Winda na Ushinde kutoka katika kampuni ya bia Serengeti na ntaitumia
kufungua duka kwani ni ndoto yangu kubwa. Na najivunia kuitumia bia ya
serengeti kwani ndio bia niipendayo na nawapongeza sana kampuni ya
Serengeti kwa kuanzisha mashindayo haya na mpaka sasa nimeshajishindia
bia nyingi pamoja na bia taslimu” alisema mshindi huyo.
Akiongelea promosheni hii meneja
wa kinywaji cha Serengeti Mr. Allan Chonjo alisema “promosheni hii ni
ya kipekee na mpaka sasa watu 110,000 wameshajishindia bia za bure na
pesa taslimu ambazo ni shilingi 10,000 na100, 000/= na droo ya kwanza
ilichezeshwa mwezi uliopita huku mshindi kutoka Moshi akiondoka na
kitita cha milioni moja, pia promosheni hii inampa fursa mshindi kununua
kile anachokitaka baada ya kujishindia fedha taslimu kwani tunaamini
baadhi ya wateja wetu wana ndoto nyingi sana za mafanikio ila tatizo
huwa ni pesa ili kitimiza ndoto zao.
Lengo la kampuni yetu ni kuendeleza umoja
na mshikamano na wateja wetu kwa kuutambua na kuuthamini mchango wa
wateja wetu kwani wao ni muhimili mkubwa katika kukuza na kuendeleza bai
yetu ya Serengeti. Na sasa kampuni ya Serengeti inachezesha promosheni
hii kutimiza azma yake ya kuinua uchumi wa wateja wao kama sehemu ya
shukrani kwa wateja wake.
Ni
wakati wako ndugu mteja kushiriki mara nyingi uwezavyo na kuhakikisha
unajishindia zaidi ya milioni saba. Ili kushiriki unatakiwa kufungua
chini ya kizibo cha bia ya Serengeti na utakuta namba maalumu na unatakiwa kuituma kwenda namba 15317 na utapokea majibu.
Tafadhari kunywa kistaarabu na ni maalum kwa 18+
No comments:
Post a Comment