Hii
Kutoka Burundi, Bi Lydia Nsekera ametengeneza Historia Ijumaa iliyopita
baada ya kuchaguliwa kuwa Mwanamke wa Kwanza kuwa Mjumbe Wa Kudumu
Katika Kamati Ya Utendaji Ya FIFA Kuwa Awamu Yote. Nsekera
amechaguliwa kuwepo kwenye kamati hio kwa muda wa miaka 4 Na Atafanyia
Kazi zake Mauritius. Wakati huo wanawake wengi wawili Moya Dodd kutoka
Australia Na Sonia Bien-Aime kutoka Turks Na Visiwa Vya Caicos Wamepewa
Awamu Ya Mwaka Moja Kwa Kila Mtu.
Nsekera
alishawahi kuwa mwanamke wa kwanza kupewa kazi hio kwa mwaka mmoja tu na
sasa amechaguliwa kwa miaka minne. Kwa sasa patakuwa na wanawake watatu
kwenye kamati hio tofauti na miaka miwili iliyopita hapakuwa na hata
moja. Hii imeonekana kama hatua nyingine kubwa ya Usawa Wa Kijinsia
Unaofanyika na FIFA. Ila kazi bado kwani kamati ina watu 24 na wanawake
ni watatu tu. Imechukua miaka 109 kufikia hapa alisema Rais wa FIFA Sepp
Blatter.
No comments:
Post a Comment