By Pascal Mayalla
Tanzania
imeshinda tuzo tatu za juu za ubunifu katika Utumishi wa Umma, barani
Afrika, kufuatia Tasisi tatu za Tanzania, kushinda nafasi ya kwanza, na
kukabidhiwa vikombe vya ushindi na rais wa Ghana, wakati wa kilele cha
maadhimisho ya Siku ya Utumishi wa Umma barani Afrika, yaliyofanyika
jana mjini Accra nchini Ghana.
Taasisi
za Tanzania zilizoshinda ni Ofisi ya Ukaguzi ya Taifa, (NAO), Wakala wa
Vipimo, (WMA), na Wakala wa Vitambulisho vya Taifa, (NIDA) kufuatia
kufanya vizuri katika maonyesho ya siku 7 ya shughuli mbalimbali za
utumishi wa umma yaliyofikia kilele tarehe 23/06/2013.
Akiuzungumzia
ushindi huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma, Mhe. Celina Kombani, amezipongeza taasisi hizo, zilizolitea sifa
taifa hili na kuelezea kufarijika kwake na ushiriki wa mkubwa wa Tasisi
za Tanzania katika maonyesho hayo ambapo jumla ya taasisi 42 kutoka
Tanzania, zilishiri.
Akisoma
hotuba katika kilele cha maandimisho hayo, Mhe. Kombani ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Mawaziri wa Utumishi Barani Afrika, amewataka watumishi wa
umma kote barani Afrika, kuwatumikia wananchi kwa bidii,
unyenyekevu, uadilifu wa hali ya juu, na kueleza utumishi wa umma ni kuwatumikia watu.
Kwa
upande wake, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma, Bw. Gearge Yambesi, amekiri kuwa Tanzania ni moja ya
nchi zinazofanya vizuri sana katika utumishi wa umma barani Afrika,
hali inayofanya Tanzania kujijengea heshima kubwa barani Afrika
na Ulimwenguni kwa ujumla.
Wakizungumzia
kuhusu ushiriki wa Tanzania katika maonyesho hayo, Waziri , Mhe. Celina
Kombani, na Katibu Mkuu, Bwana. George Yambesi, wanaeleza zaidi.
Akizungumzia
maonyesho hayo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Press and Public Relations
(PPR), Bw. Pascal Mayualla, amesema mfulululizo wa vipindi vya redio na
Televisheni, kuhusu ushiriki wa Tanzania, katika Maonyesho ya Utumishi
wa Umma barani Afrika, vitaanza kuonekane kesho, katika vituo mbalimbali
vya redio na Televisheni.
No comments:
Post a Comment