Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, June 25, 2013

VIONGOZI WATANO WA CHADEMA WASHITAKIWA KWA UGAIDI TABORA .... MAJINA YA VIONGOZI HAO HAYA HAPA


Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Dar es Salaam na vijana wengine leo wameshtakiwa kwa Ugaidi katika mahakama ya Hakimu mkazi Tabora mjini.

Mbali ya Kileo, vijana wengine wa Chadema, ni Evodius Justinian wa Buboka, Oscar Kaijage wa Shinyanga, Seif Magesa Kabuta wa Mwanza, Rajab Daniel Kihawa wa Dodoma, jana wamesomewa shitaka la Ugaidi kwa kumteka na kumwagia tindikali Musa Tesha katika kampeni za Uchaguzi mdogo wa Igunga uliofanyika mwaka 2011.
Watuhumiwa hao walisomewa mashtaka mawili wote, la kwanza ni la kufanya ugaidi, na la pilini kumwagia tindikali Musa Tesha.

Kesi hiyo ilikuwa ilisikilizwa mbele ya hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, ya Tabora Mjini,Joktani Rushwera, huku upande wa serikali ukiwakilishwa na Wakili Juma Massanja na Ildefons Mukandara Baada ya kusomewa shitaka hilo, Upande wa utetezi wa ukiongozwa na wakili Prof Abdalah Safari, ukiwajumlisha Peter Kibatala na Gasper Mwalyela ulitoa hoja kuiomba mahakama hiyo ifutilie mbali mashtaka hayo kwa sababu, kwanza mashtaka hayakuwa na uhai kwa kuwa yamefunguliwa bila ridhaa ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini.

Sheria za uendeshaji wa makosa kama hayo hapa nchini zinadai kuwa mashataka kama hayo yanapofunguliwa ni lazima ridhaa ya Mkurugenzi wa mashtaka iwepo. Kwa kuwa ridhaa hiyo haikuwepo, mawakili waliiomba mawakili kuitupilia mbali kesi hiyo.


Sababu ya pili iliyotolewa na upande wa Utetezi ilikuwa kwamba maelezo ya kesi kuwa ni ya ugaidi, yalikuwa hayaonyeshi kuwa ni ya kigaidi tofauti na makosa mengine ya kawaida kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, hivyo waliiomba Mahakama kutupilia mbali shitaka hilo au lifunguliwe kama kosa la kawaida.

No comments:

Post a Comment