Pages

Wednesday, June 5, 2013

WATU SITA WAZIMIA WAKATI WAKIAGA MWILI WA MAREHEMU ALBERT MANGWEA.

tunaomba radhi kwa picha

WATU sita wameanguka na kupoteza fahamu wakati wa kuuaga mwili wa aliyekuwa msanii wa muziki wa Kizazi kipya nchini Tanzania katika viwanja vya Leaders Club, watu hao ni wanawake wanne na wanaume wawili na wanaendelea kupewa huduma ya kwanza kutoka kwa kikosi cha msalaba mwekundu waliopo katika viwanja hivi na kuwapa huduma ya kwanza.

Mwandishi wa Habarimpya.com akiwa katika viwanja hivyo jijini Dar es Salaam anasema kwamba umati mkubwa umezidi kuongezeka katika viwanja hivyo huku vilio vikitawala.

Wasanii wa muziki wa Kizazi Kipya wakiongozwa na msanii maarufu Abdul Nassib (Diamond Platinumz) wamejitokeza kwa wingi katika tukio hilo kihistoria katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya.

Akizungumza na Habarimpya.com katika viwanja hivyo msanii aliyewahi kutamba na kibao chake cha kwanza cha Zeze langu T.I.D ambaye kwa sasa anatamba na Bendi yake ya muziki ya Top Band amesema kwamba, "Kuna mipango mingi tulipanga na Mangwea lakini leo nasikitika sana kuona nimebaki peke yangu".

No comments:

Post a Comment