Pages

Sunday, June 30, 2013

ZIARA YA OBAMA- MAENEO YATAKAYOATHIRIKA


 
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, SAID MECK SADICK, amesema serikali imechukua tahadhari zote katika kuhakikisha shughuli zote za wananchi za kibiashara zinaendelea kama kawaida wakati wa ziara ya rais wa Marekani Barack Obama.
Aidha mkuu huyo wa mkoa amesema katika kipindi hicho wafanyabiashara kutoka mikoani na ndani ya jiji wataendelea kuingiza bidhaa zao katika masoko kama kawaida bila kuzuiliwa, na kwamba si barabara zote zitakazofungwa na kutolea mfano wa barabara itakayofungwa kuwa ni barabara ya Nyerere ambayo wageni wengi hutumia na kwamba ziara hiyo haitaathiri maonesho ya 37 biashara maarufu kama sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. JULIUS NYERERE.

Rais wa Marekani Barack Obama anatarajia kuzuru Tanzania siku ya jumatatu ambapo miongoni mwa masuala atakayoangazia ni pamoja na kuhamasisha demokrasia na kukuza fursa za kiuchumi.

Maandalizi ya mapokezi ya Rais Obama yamezidi kupamba moto hasa katika jiji la Dar-es salaam ambapo ndipo kituo chake cha kwanza kwa rais huyo nchini Tanzania huku suala la usafi na matengenezo katika barabara nyingi Jijini likionekana kupewa kipaumbele tofauti na siku zote.

No comments:

Post a Comment