Zitto Kabwe amefunguka na kudai kuwa kwa sasa wanajiandaa
kufanya mapinduzi ya nchi endapo serikali watu walioficha
mabilioni uswiswi hawatashughulikiwa ipasavyo....
Suala
la baadhi ya Watanzania kuhifadhi mabilioni ya fedha nchini Uswisi
limechukua sura mpya, baada ya tume maalumu kuwahoji vigogo 200 wakiwamo
wabunge, wanasiasa na wafanyabiashara.
Habari
zilizopatikana zinaeleza kuwa tume hiyo inayoongozwa na Mwanasheria
Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema tayari imeshafanya kazi hiyo kwa
miezi miwili sasa.
Tume hiyo maalumu iliyoundwa na Serikali kwa Azimio la Bunge
lililotolewa mwishoni mwa mwaka jana, inatarajiwa kukamilisha uchunguzi
huo wakati wowote kuanzia sasa na kuwasilisha ripoti hiyo katika kikao
kijacho cha Bunge.
Zitto Kabwe anatoa angalizo katika hatua hiyo ya jaji Werema
kwa kusema kuwa hatua hii isiwe "zima moto" na daganya toto
ili kuwafumba macho watanzania...
Ubabaishaji wowote kwa mujibu wa Zitto Kabwe utasababisha mapinduzi ya nchi.....
Hii ni post yake aliyoweka katika mtandao wa twitter
No comments:
Post a Comment