Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, July 3, 2013

AJALI YA BUS LA SAI BABA WATU 21 WAMEJERUHIWA VIBAYA NA WENGINE 30 WANUSURIKA KIFO

 
 
 
 
 
 
  
watu 21 wamejeruhiwa vibaya na wengine 30 wakinusurika kifo baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka jijini Dar es salaam kwenda Songea kupata ajali eneo la vigwaza mkoani pwani.
 akizungumza na MCHOME BLOG mkuu wa kikosi cha askari wa barabarani Chalinze Assistance Inspector Sule amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa mbili asubuhi ya leo July 02 baada ya basi la abiria la kampuni ya Saibaba lenye namba za usajili T 779BKL kutaka kulipita gari lingine huku likiwa katika mwendo kasi na hatimaye gari lilimshinda dereva huyo na kisha kupinduka
 
Aidha ameongeza kuwa majeruhi hao wamekimbizwa katika hosiptali ya tumbi kibaha kwaajili ya matibabu,basi hilo lilikuwa na jumla ya abiria 51.
 
Habari kwa hisani ya www.mchomeblog.com

No comments:

Post a Comment