Pages

Saturday, July 20, 2013

ANGALIA PICHA::NGUO FUPI NUSURA ZIWATOKEE PUANI WAREMBO HAWA

Warembo hao wakikimbia baada ya kuanza kuzomea na wananchi.
Mmoja wa warembo hao akimsubiri mwenziye ajisitiri na yeye achague nguo.
...Na mwenzake akijaribu nguo ya kumsitiri.
...Baada ya kujisitiri.
...Wananchi wakiwashangaa wasichana hao waliotaka kuwavurugia mfungo.
WASICHANA wawili wasiofahamika mara moja nusura wakumbwe na sekeseke la aina yake kutoka kwa ‘watoto wa mjini’ baada ya kupita mtaani na vivazi vifupi.
Kituko hiko kilianzia maeneo ya Kivukoni jijini Dar ambapo wasichana hao walipanda kivuko na kushukia Kigamboni, wakitembea bila kujali watu waliokuwa wakiwaangalia na kuwazungumzia.
Hata hivyo baada ya kuwaona watu wanaanza kuwazomea walikimbilia katika maduka ya nguo yaliyopo karibu na kujifunika kwa nguo za kistaarabu kisha wakaendelea na safari zao.
Watu waliokuwa karibu na eneo hilo walisema kuwa wasichana hao wasingefika mbali pasipo kufanyiwa ‘kitu mbaya’ kwani walizidi kujiachia bila kujali kuwa huu ni Mwezi Mtukufu hivyo si vizuri kuvaa nguo za ajabu kiasi hicho hata kama si waumini wa dini hiyo.
(PICHA NA CHANDE ABDALLAH / GPL)

No comments:

Post a Comment