Pages

Thursday, July 18, 2013

Benedict Charles Lukumay wa Club Masai Afariki kwa Ajali ya Gari

Marehemu Benedict (Kulia)
Habari nilizozipata muda mchache uliopita na kuthibitishwa na ndugu na jamaa wa karibu zinasema Benedict Chalres Lukumay amefariki kwa ajali ya gari eneo la Mikumi mkoani Morogoro usiku huu.

Chanzo cha kifo chake kimeelezwa kuwa ni ajili ya gari iliyotokea eneo la Mikumi mkoani Morogoro majira ya saa mbili usiku.

Meneja mkuu wa Meridian Hotel LTD Mzee Mponda amethibitisha juu ya kifo hicho, huku akinieleza kuwa ilitokana na ajali ya gari.

"Wakiwa na mwenzake aliyefahamika kwa jina la Adrian na gari binafsi wakielekea mkoani Iringa gari aliyokuwamo marehemu iligonga nyuma roli lililokuwa limesimama njiani." alisema Mzee Mponda.

Adrian ambaye ndiye aliyekuwa anaendesha gari alinusurika kwenye ajali hiyo.

Benedict alikuwa ni mmoja kati ya Wakugenzi watendaji wa kampuni ya Meridian Hotel LTD inayomiliki na kuendesha kumbi za burudani zikiwemo Masai Kinondoni, Masai Ilala na Masai Galapo Ilala.

Kifo chake kimeacha pengo kubwa si tu kwa familia bali hata wapenda burudani, akifahamika kimchango katika kusimamia na kuendeleza burudani na yakiwemo maonyesho mbalimbali ya wanamuziki wa bongo fleva na fani nyinginezo.

Mungu alaze Pema ROHO ya Marehemu Ben.....

No comments:

Post a Comment