Pages

Thursday, July 4, 2013

GIGGS APEWA UKOCHA MANCHESTER UNITED

:


 Meneja mpya wa Manchester United David Moyes amemteua kiungo mkongwe Ryan Giggs kuwa kocha-mchezaji wa timu hiyo ya Old Trafford leo mchana.
Giggs, 39, ambaye ni kati ya wachezaji waliotunukiwa nishani nyingi sana katika soka la Uingereza, amekuwa akifanya mitihani yake ya ukocha na anatarajiwa kupata leseni ya ukufunzi ya UEFA mwaka kesho.
Mnamo Machi mwaka huu, Giggs aliongeza mkataba wake wa kuchezea Mashetani Wekundu kwa mwaka mmoja, na anatarajia kubeba majukumu kamili kama kocha na mchezaji wa kikosi cha kwanza cha Man U msimu huu. PICHA | AFP

No comments:

Post a Comment