Pages

Tuesday, July 9, 2013

Hawa Ndio Wasanii Wakubwa Duniani Waliobadilisha Sura na Maumbile yao Kwa Upasuaji.



TinaTurner alifanyiwa upasuaji wa pua ambapo mwenyewe amekubali hilo.Hiyo ilikuwa ni kutokana na manyanyaso na kipigo alichokuwa akipata kutoka kwa mumewe
Ike na kusababisha mfupa wa pua kuvunjika na hivyo 

kupelekea yeye kufanyiwa upasuaji huo.

Kuna habari za chini chini kuwa amefanyiwa upasuaji wa kunyanyua ngozi ya uso wake kwasababu licha ya 
kuwa na umri mkubwa Tina anaoneka mrembo bado!
Joan Rivers amefanyiwa upasuaji mara nyingi
kurekebisha sura yake.Amesema kwa sasa hahitaji kufanyiwa upasuaji tena!

Madonna amefanya marekebisho katika uso wake. Kaka
yake Madonna alikubali kuwa Madonna alifanya upasuaji wa kunyanyua ngozi ya uso wake kiasi cha kumfanya yeye(kaka yake),kushindwa kumtambua
Madonna.

Mel BNyota wa iliyokuwa Spice Girls Mel B ana
umbo lenye mvuto.Nyota huyu alifanyiwa upasuaji kuongeza ukubwa wa matiti yake.
Uongezwaji wa matiti ulimletea matatizo na kuamua yaondolewe. Pamoja na
hivyo Mel B bado anaonekana ni
mrembo.

Michael Jackson
Mengi yaliandikwa kuhusu marekebisho yaliyofanyika
katika uso na ngozi ya nyota huyu.Inasadikiwa kuwa Michael alifanyiwa upasuaji mara kadhaa kupunguza ukubwa wa pua yake!Rangi ya ngozi yake nayo ilibadilika kama picha ionyeshavyo!
 
Queen Latifah
Kutokana na maimivu ya mgongo na mabega aliyokuwa nayo Queen Latifah,ilimpelekea afanyiwe upasuaji kupunguza ukubwa wa matiti yake
hivyo Queen Latifah alifanyiwa upasuaji si kwa ajili ya sababu za urembo!



Jermaine Jackson amefanyiwa upasuaji wa kurekebisha pua na marekebisho katika ngozi yake.

No comments:

Post a Comment