Stori: Imelda Mtema
MAAJABU
yameibuka kwenye mazishi ya baba mzazi wa Mtangazaji wa Kipindi cha
Wanawake Live kinachorushwa hewani na Televisheni ya East Africa,
Joyce Kiria, Michael Francis Iwambo Kiria kufuatia kuchimbwa kwa
makaburi mawili, Amani lina mkasa mzima.
Tukio
hilo la ajabu lilitokea kwenye msiba wa mzee huyo, Kata ya Kibosho,
Kijiji cha Dakau, mkoani Kilimanjaro wakati wa maandalizi ya kuuhifadhi
mwili wa merehemu huyo.
Mzee
Kiria alifariki dunia Julai 10, mwaka huu jijini Tanga alikokuwa akiishi
na mke mwingine (si mama’ke Joyce) baada ya kuugua ghafla.
KWA NINI MAKABURI MAWILI?
Ilielezwa
kwamba ndugu wa mzee Kiria waliopo kijijini Dakau walipopata taarifa za
kifo cha mzee huyo na kwamba mwili wake utazikwa kijijini hapo
walichimba kaburi kwenye eneo la makaburi ya ukoo.
“Maiti
ilifika kijijini, taratibu za ibada zilifanyika kanisani, lakini kazi
ikawa kwenye kuupeleka mwili kaburini. Mke wa marehemu aliyekuwa akiishi
naye Tanga aliuliza eneo lililochimbwa kaburi na kuambiwa ni la ukoo,
akasema haiwezekani azikwe hapo. NA GPL
“Mwanamke
huyo alisema marahemu wakati wa uhai wake aliagiza akifa azikwe kwenye
shamba alilopewa na baba yake mzazi, mzee Francis Kiria na si
vinginevyo,” alisema mpashaji wetu aliyekuwa eneo la tukio.
MSIBANI HAPAKALIKI
Vuta
nikuvute ilitokea eneo la msiba, mke wa marehemu aliweka wazi msimamo
wake kwamba endapo ndugu watalazimisha marehemu azikwe eneo la familia
angeondoka na maiti kurudi nayo Tanga kwa mazishi.
JOYCE KIRIA AMWAGA MACHOZI, APIGA MAGOTI
Ilibidi
ndugu waweke kikao cha dharura cha familia ili kumshawishi mwanamke huyo
akubaliane na matakwa ya familia kwa sababu ndugu wote walizikwa
makaburi ya ukoo, lakini mjane huyo alitia ngumu.
“Yule mke
wa marehemu alikataa katakata, alisema lazima mume wake azikwe kwenye
shamba alilopewa na baba yake kama alivyotaka akiwa hai.
“Ilifika
mahali, Joyce Kiria alimpigia magoti mwanamke huyo huku akilia na
kumuomba aruhusu baba yake azikwe kwenye kaburi lililokwisha chimbwa
kwenye eneo la ukoo, lakini wapi, mwanamke aligoma,” alizidi kusema
mpashaji wetu.
KABURI LA PILI LACHIMBWA
Kwa
mujibu wa mtoa habari wetu, baada ya msimamo wa mwanamke huyo kusimama
kwenye maamuzi, ilibidi ndugu wakubaliane naye kwa kutuma watu kwenda
kuchimba kaburi la pili kwenye shamba la marehemu.
Cha
ajabu, wakati wachimbaji wakiendelea na zoezi hilo, kondoo mmoja mweupe
alianza kulia kwa muda mrefu jambo lililowashangaza watu walioshuhudia.
Wengi wa
watu hao walihoji kilio cha kondoo huyo wakisema huenda aliashiria mambo
fulani ambayo wazee wa kimila ndiyo wanatakiwa kufuatilia na kutoa
ufafanuzi.
Mbali na
kilio cha kondoo huyo, baadhi ya watu walisikika wakisema wanaamini
baada ya mazishi hayo, kifo kingine kitajiri kwa sababu haijawahi
kutokea kijijini hapo makaburi yakachimbwa mawili kwa ajili ya marehemu
mmoja.
WAZEE WA KIMILA WAKAA KIKAO
Kufuatia
kuwepo kwa makaburi mawili, habari zinasema ilibidi wazee wa kimila
kuketi kikao cha ghafla na kuulizana mila na desturi za mababu ni nini
inapotokea hali kama hiyo.
Ndipo
mzee mmoja alisema lazima kondoo mmoja mweupe achinjwe kisha damu yake
kumiminiwa ndani ya kaburi lisilotakiwa halafu mzoga wa kondoo huyo
ufukiwe katika kaburi.
Kondoo aliyepata ‘kura nyingi’ ni yuleyule aliyelia baada ya mjane wa marehemu kushinda eneo la kuzikiwa mume wake.
KONDOO AKAMATWA, ASOGEZWA KABURINI, ACHINJWA
Kondoo
huo alikamatwa, akasogezwa jirani na kaburi, akachinjwa mpaka kukata
roho. Damu yake ilimiminikia kaburini, nyingine ilikingwa kwenye kikombe
na kumiminiwa kaburini halafu mzoga wake ukatupwa humo na kufukiwa.
BABA WA JOYCE AZIKWA SASA
Baada ya
kufanyika kwa mambo hayo yote, mwili wa marehemu ukiwa ndani ya jeneza
la mbao lenye rangi ya damu ya mzee ulipelekwa kuzikwa kwenye kaburi
lililochimbwa shambani kwake.
Mazishi
yalifanyika kwa amani, baadaye waombolezaji walitawanyika kurudi eneo la
msiba lakini gumzo kuu likiwa kuchinjwa na kuzikwa kwa kondoo huyo.
Baadhi ya
watu kijijini hapo wenye rika la utu uzima, walisikika wakisema
hawajahi kuona mnyama akitolewa kafara ya kifo cha binadamu.
Wengi walisema wanachokijua wao ni kwamba, utata wa kaburi humalizwa kwa kuzikwa mgomba au majani yaitwayo isale.
JOYCE KIRIA ANENA
Baada ya
kupata habari hiyo ya kusisimua, juzi Amani lilimtafuta Joyce Kiria ili
kuthibitisha kutokea kwa habari hiyo na kumpata nyumbani kwake,
Changanyikeni, jijini Dar ambapo alikiri na kusema hata yeye mwenyewe
haelewi kitu ambacho kimetokea kwa sababu hajawahi kuona katika maisha
yake.
“Kwa
kweli hayo ni majaabu kwangu, hata mimi nimeshangaa kupita kiasi,
sijawahi kuliona jambo hili katika maisha yangu na limeniumiza kupita
kiasi,” alisema Joyce huku machozi yakimlengalenga.
No comments:
Post a Comment