Pages

Saturday, July 20, 2013

HIZI NDIO BEI ZA TIKETI ZA KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014: YA BEI YA CHINI KABISA NI $220 MECHI YA UFUNGUZI - FAINALI NI $440

Bei za tiketi kwa ajili ya mashabiki wa kutoka nje ya Brazil watakaokwenda nchini Brazil kuangalia fainali za kombe la dunia zitaanzia bei ya $90 (£59, 69 euros) kwa mechi za makundi.
FIFA imetangaza kwamba tiketi ya bei rahisi kabisa kwa mashabiki wataokwenda Brazil kwa ajili ya mchezo wa fainali ya michuano hiyo itaanzia $440 (£288) na ya bei ghali kabisa itakuwa kiasi cha  $990 (£650) ambayo ni sawa na 1,603,800 kwa fedha za madafu.

Michuano hiyo itaanza mnamo tarehe 12 June mwaka ujao, huku mechi ya kwanza ya ufunguzi ikichezwa jijini Sao Paulo.

Tiketi zitaanza kuuzwa mnamo 20 August mwaka huu.
Mashabiki wana muda mpaka 10 October kutuma maombi ya kununua tiketi na utafanyika uchaguzi wa kuamua maombi yapi yamepita.


Kuna jumla ya tiketi millioni 3 ambazo zipo kwa ajili ya maombi ya manunuzi ya mashabiki. 

BEI ZA TIKETI ZA KOMBE LA DUNIA (Mashabiki wa nje ya Brazil)

Matches Category 1 Category 2 Category 3

Opening Match $495 $330 $220
Group Matches $175 $135 $90
Round of 16 $220 $165 $110
Quarter Finals $330 $220 $165
Semi Finals $660 $440 $275
3rd / 4th Place Match $330 $220 $165
Final $990 $660 $440

Kwa raia ya wa Brazil tiketi ya bei rahisi kabisa itaanzia kwenye kiasi cha $15. Hizi zinapatikana kwa wanafunzi tu, na wale watu wenye umri zaidi ya miaka 60 ambao wapo kwenye mipango ya kusaidia jamiii. Kwa wabrazil wengine wote bei ya chini kabisa itaanzia kiasi cha $30. 

Bei ya chini kabisa ya tiketi katika michuano ya kombe la dunia mwaka 2010 nchini South Africa ilikuwa ni  $20, na pia ilikuwa kwenye mechi za  makundi.
FIFA mwanzoni ilisema kwamba tiketi za kombe la dunia mwaka 2014 zitakuwa za bei rahisi kuliko zote.

Katika mtandao rasmi wa kuuza tiketi wa FIFA kutakuwepo na ramani ya ya uwanja inayokuonyesha sehemu za kukaa kutokana na bei ya tiketi yako.
Hi inamaanisha kwamba hakutakuwa na kuhangaika katika kujua ni wapi unapaswa kukaa, alisema mkurugenzi wa masoko wa FIFA  Thierry Weil, ambaye ndio anayehusika na masuala ya yote tiketi.

Mashabiki wanaweza kuomba angalau siti nne kwa mechi, na kwa mechi saba tu.
Amesema pia kutakuwa na mfumo wa kuuza tena tiketi ikiwa watu waliomba au kununua tiketi kabisa na wakashindwa kufika uwanjani. 
Angalau tiketi 400,000 zitawekwa maalum kwa mashabiki wa nchi mwenyeji, huku karibia tiketi 50,000 zikiwa maalum kwa ajili ya wajenzi wanaojenga viwanja vitakavyotumika kwenye michuano hiyo.

KWA NDUGU ZANGU WABONGO MNAOTAKA KUOMBA KUNUNUA TIKETI UNAWEZA KUINGIA KWENYE MTANDAO HUU - www.ticket.org/WorldCup

No comments:

Post a Comment